Posts

Showing posts from May, 2025

1. Hosiana! Asifiwe

Hosiana asifiwe ajaye kwa jina la bwana! Hosiana mbinguni! Anakuja kwajina la Bwana, Anakuja kwa jina la Bwana, Hosiana! Hosiana! Hosiana mbingunui Hosiana mbinguni

2. Hosiana, Mesiya

  Hosiana, Mesiya Aingia mjini kwake Fagieni popote, Zipambeni njia zote; Tandikeni mauwa, Aingie na shwangwe. Hosiana,Mwokozi Njoo, twakungojea Bwana. Tumepamba nioyo, Twakukaribisha kwetu. Tunakufungulia, milango ya mioyo Hosina, ee shujaa! Utusaidie sisi, Tuwe wako kwa kweli Tukutumikie vema. Kwani hutakubali Watu wasio kutii. Hosiana, Mfalme mkuu! Uingie kwetu hima! Uliebarikiwa, Uingie mlango wetu. Hosiana, karibu! Bwana, njoo! Haleluya!

3. Sayuni, ufuhi!

Sayuni, ufurahi! Shangilia yerusalemu! Yuaja mfalme wako, Mwenye amani kwako. Sayuni hufurahi! Shangilia yerusalemu. Hosiana, Mesiya Utubariki sasa. Jenga ufalme wako Ulimwenguni mwote. Hosiana, Mesiya Utubariki sasa. Hosiana! Pongezi! Twakuamkia bwana! Kiti cha enzu yako Chasimama milele. Hosiana! Pongezi! Twakuamkia Bwana!

4. Fungua Milango Yote

Fungua milango yote Yuaja Bwana wa mbingu, Mfalme wa wafalme wote, Mwokozi wa ulimwengu. Atuletea uzima; Kwahiyo tumuimbieni; Tumsifuni Mungu, Aliye tuumba. Ni mwenye haki na shujaa Uple mwingi amevaa; Rehema ni taji yake; Huruma ni fimbo yake; Atuondolea shida. Kwahiyo tumuimbieni; Tumsifuni Mungu, Mwokozi watu mkuu. Miji na nchi Huchipuzwa, Afikako Mfamle huyu; Nayo mioyo huchekeshwa, Anayo ingia Yesu. Ndio jua la furaha Linalo tufurahisha. Tumsifuni Mungu Mtunza mioyo yetu. Fungua milango yote! Tengenezeni mioyo! Makuti yawe upole, Furaha, pendo, amni. Mwokozi ata wajia, Aleta raha, uzima. Tumsifuni Mungu, Ni mwenye rehema. Njoo, mwokozi wangu Yesu, Nakufungulia moyo. Uingie na rehema, Nione upole wako. Uniongoze kwa roho, Nifike kwako Mbinguni. Jina lako Bwana Lisifiwe pote.

5. Nikulakije Vema

Nikulakje vema Bwan wangu Yesu Wote wanakungoja Wapewe uzima. Nuru yako ing’aze Hata moyo wangu. Nijue mabo mema, Yakupendezayo. Wamekutandikia Mauwa na nguo. Name nakuimbia Nyimbo za furaha. Moyo ukupendeze Kwa sifa na nyimbo, Ukakutumikie Sikuzangu zote Umetoka Mbinguni Ukawa masikini Ukaacha fura Utupe uzima. Natulipo nyang’anywa Ufalme na raha, Ukaja mponya wetu Kuturudishia. Nalifungwa na mwovu, Ukanifungua. Nikawa nimetwezwa, Ukanitukuza, Ukanifanya mkubwa, Ukanipa mali, Zisizo malizika, Kwa kutu na wezi. Umenijia mimi, Sababu ya nini? Sababu ya kupenda Uwaponye wote Waonao huzuni Kwa makoso yao Wakijuta kwa kweli, Utawapokea. Ushike neon hili, Umati wa Yesu, Ukiwa na huzuni Na shida popote. Usiogope kitu; Wokovu tayari. Anaye tufariji Yukaribu sasa.

6. Wakristo, Iwekeni

Wakristo, iwekeni Mioyo tayari. Yesu awaingie, Ni Mwokozi wenu. Mungu amemtuma Kwa neema na rehema Atuletee sisi Uzima na nuru. Mwokozi ana kuja, Mlimieni njia! Mioyo iwe safi Acheni matendo Yanayomchukiza. Lijazwe kila bonde, Milia ipunguzwe Mioyoni mwenu. Ukiwa mnyenyekevu, Wapendwa na Mungu. Ukiwa na kiburi, Utaangamizwa. Ukimtumikia, Mungu kwa mwendo mwema Umpendezao yeye, Yesu akupenda. Uniweke tayari Niliye maskini, Ee Yesu siku hizi Kwa rehema yako Ingia moyoni, Ukinijia sasa. Nami nitakusifu Kwa kinywa na moyo.

7. Moyo Wangu Sikiliza

Moyo wangu sikiliza Habari njema hii Ya wokovu mkubwa. Sikia kuimbwa kwao Malaika na watu: “yesu azaliwa.” Mponya amekuja leo Kutoka mbinguni, Aokoe watu. Mungu wetu ameshuka, Akawa mwana mtu Kwa ajili yetu. Na sasa yumo zizini, Aita: “njooni Hima kwangu wote, Nawaondolea ninyi Uchungu wowote, Muwe na furaha.” Basi tumwendee hima Wakumbwa wadogo, Njooni wote sasa! Awe mwanga wetu. Wenyeshida na ukiwa njooni, Awape neema yake Mungu, Yeye ana mali nyingi, Dhahabu na fedha Za mioyo yenu. Ninakaa ulimwenguni Lakini napenda Kuhamia kwako. Mwisho niwe furahani Pamoja na wewe mwenye utukufu.

8. Amekuja Mwokozi

K:   /:Amekuja W:   mwokozi.:/ K:   /: Ufalme wa juu karibu. W:   Amekuja mwokozi. :/ K:   /:Geukeni W:   mioyo. :/ K:   /:Watatupwa wenye kiburi. W:   Geukeni mioyo. :/ K:   /:Shoka lipo W:   shinani, :/ K:   /: Mti usiozaa wakatwa. W:   shoka lipo shinani.:/ K:   /:Ana ungo W:   mkononi,:/ K:   /:kupepeta ngano yake. W:   Ana ungo mkononi.:/ K:   /:Yatachomwa W:   Makapi,:/ K:   /:Ngano yawekwa chanjani. W:   Yatachomwa makapi:/ K:   /:Nabatiza W:   Kwa maji,:/ K:   /:Yeye hubatizwa kwa Roho. W:   Nabatiza kwa maji.:/ K:   /:Mbele yake W:   Sifai,:/ K:   /:Kumfungulia viatu. W:   Mbele yake sifai.:/ K:   /:Elekea W:   Mbinguni, K:   /:Kristo katufanyia njia. W:   Ya kwen...

9. Faraja, Tumaini Langu

Faraja tumaini langu Usiniache gizani, Moyo ni wazi kukungoja, Ee Yesu uniingie, Furaha ya mbingu na nchi, Mwana Adamu na Mungu; Ee nuru kutoka mbinguni, Angaza moyo wangu huu. Mototo mpendwa, Nakuomba, Chagua moyo wangu huu, Ufanye  kuwa horilako Ukalazwe humo wewe. Ili nipate mwisho mwema Wa shida yangu na vita. Zaliwa ndani yangu Yesu, Na ndani yangu ukuwe. Mwokozi wangu utulize Tumaini hili kubwa. Ukija nitakupokea Kwa roho nyenyekevu, hii. Uweza wangu wote pia Wakungojea kwa uchu. Nataka kukutumikia: Njoo, Yesu usikawie .

10. Bwana Anakuja

Bwana anakuja Twendeni kumlaki Bwana wangu wa majeshi. Iwasheni mioyo Tukampokee Huyo mwenye utukufu. Karibu Bwana, njoo Karibu Bwana, njoo Shinda pamoja nasi. Wewe ndiwe mfalme, Mfale wa mbinguni Utulishe wenye njaa. Wewe ndiwe mwanga, Sisi tu vipofu Tufanye tuone tena Wewe ndiwe njia, Tuta kufuata Turudi kwa baba yetu. Wewe ndiwe kweli, Utuangazie Tusije tukapotea. Hosanna, Hosana, Huyo mbarikiwa Anakuja kwetu sisi. Aja kutulisha na kutugawia Matunda ya ukombozi.

11. Natoka Leo Mbinguni

Natoka leo mbinguni Naleta habari njema Habari yenye furaha Kwaninyi na watu wate. “Amezaliwa kitoto Na mwana mwali Maria, Nimototo mzuri na mwema, Awaletea furaha.” Ni Yesu, mwana wa Mungu, Mwokoxi wa ulimwengu Atakae kuondoa Makosa yote na shida Awapa wote wokovu Ulio wekwa naMungu Make nanyi mbinguni Pamoja nasi milele Alama yenu iwe hii; Zizini mototo wa maskini Alie vikwa viguo, Nae ni Bwana wa mbingu Tumsifuni sisi sote, Tuwafuate wachunga, Tuyaone yale makuu, Tulio pewa na Mungu. Yesu unipendezae, Ugeuze moyo wangu, Uwe nyumba yako nzuri, Nisikuwache daima. Tumsifu bwana wa mbingu, Alie mtoa mwanawe. Tumimbie kwa furaha Pamoja nao malaika.

12. Njooni, Tumheshimu Yesu

Njooni, tumheshimu Yesu, Tumtolee sifa zetu, Tumwimbie kwa furaha, Sisi watu wa Yesu. Baba amemtuma Mwana Atuletee uzima, Utakao pewa watu Wenye shida  na kufa. Moyo wake watupenda Kwa upendo amekuja, Aokoe wenye dhambi Wasishindwe na mwovu. Nuru imetutokea, Yesu akiponda kichwa Cha adui wetu mkali Anayetudanganya. Tuta barikiwa kweli, Tukishika neon hili, Tukimsifu Bwana Yesu Kwa vyinywa na mioyo. Mwana mzuri Bwana Yesu, Twakuomba tupeleke Pale wakuimbiapo Malaika nyimbo nzuri

13. Salamu, Yesu Bwanangu

Salamu, Yesu Bwanangu Wewe uzima wangu Nimekujia, naleta Vyote ulivyonipa: Ni moyo na mwili wangu Ndiyo heshima yangu. Umezaliwa Bwanangu Kwa ajili ya mimi; Umenipenda kabisa, Umenipa wokovu. Tangu mimi sijaumbwa Umenitengenezea Ukombozi wa moy. Uvuli mzito wa mauti Ulinifunika: Umenitokea jua, Waniangaza moyo. Wewe bwana umenipa Nuru, raha na uzima. Nakushukuru Bwana.

14. Siku ya Furaha (Aliyozaliwa Yesu)

Siku ya furaha, siku ya Uzima aliyozaliwa Yesu. /:Tulipotea, Yesu akaja. Furahini, furahini, Wakristo!:/ Siku ya furaha, siku ya Uzima aliyozaliwa Yesu. /: Yesu ashuka, atuokoe. Furahini, furahini, Wakristo!:/ Siku ya faraha, siku ya Uzima aliyozaliwa Yesu. /: Malaika wote wamsifu Mungu Furahini, furahini, Wakristo!:/

15. Tawi Limechipuka

Tawi limechipuka Shinani mwa Yese, Kama tulivyopashwa Habari na wazee. Likatoa ua Wakati wa usiku Lilipochanua. Isaya alitaja ua hilo zuri. Ni Yesu, mponya wetu, Maria alimzaa Usiku mtulivu. Uwezo wake Mungu Umefanya hivi. Na ua hili dogo Lanukia vyema; Lang’aa kama jua Giza lakufukuzwa. Ni Mwana wa Mungu, Hata mwana Adamu; Mwokozi wa watu. Siku ya kufa kwetu Yesu tuongoze, Tuiache dunia, Twende furahani Mbinguni kwa Mungu Pale tuta kusifu Pasipo kukoma.

16. Tunakuamkia Yesu

Tunakuamkia Yesu Tunakupa pongezi. Umezaliwa kikiwa, Malaika wakuabudu, Uwe nasi! Mwana na Mungu wa pekee, Yeye ni mgeni wetu, Anajiunga na sisi Mfalme wa kale na kale! Uwe nasi! Ashikaye ulimwengu Ashikwa na Maria! Ni mtoto  mdogo na mchanga! Tena ni Bwana wa mbingu! Uwe nasi Nuruu ya milele aja Kuleta mwanga wake Aondoa giza lote; Tuwe watoto wa mwanga. Uwe nasi! Kwetu akawa maskini Kwa kutuhurunia, Tupate mali ya mbingu, Tuwe watoto wa Mungu. Uwe nasi! Amefanya haya yote Kwa kuwa atupenda. Kwa hiyo furahini tu Na tumshukuru daima! Uwe nasi!

17. Tuimbe na Kusifu

Tuimbe na kusifu nyimbo za furaha: Yesu Bwana wetu Zizini Bethlehemu, Furha ya mioyo. Mponya na Mwokozi, Tunakusifu. Nakutumaini sana, Uliye juu. Ee Mwokozi mwema Tuliza moyo wangu, Unipe neema yako, Kitoto ch huruma. Univute juu,univute juu.

18. Umati wa Yesu

Umati wa yesu, njooni kwa furaha Msikie habari ya sikukuu! Mwana wa Mungu Azaliwa kwetu. Njooni tumtukuze! Njooni tumtukuze! Njooni tumtukuze! Yesu Kristo! Rehema zake Mungu Ni nyingi,alimtuma Mwana wake Yesu, Awakomboe watu, Kwetu ni kwa Mungu, Kwetu kwa Mungu. Na watu wakaao Katika giza wote Wanakungojea Wewe Mwokozi wetu, Na kukufurahia Uliyetukomboa. Yesu Bwana wetu Tunakutukuza. Mbinguni malaika Wamwimbia wote Na wote wakaao kwake Mungu. Mungu ni mkuu, Aliyetupenda Njooni tumtukuze! Tumsifu mwokozi yesu Siku zote, Aliyezaliwa kwetu leo. 19. Usiku Mtakatifu! Usiku mtakatifu! Wengine walala Wakeshao ni yosufu tu Na Maria waliomlinda Yesu mwana mzuri Yesu mwana mzuri.

20. Njooni Wachungaji Bethlehemu!

Njooni wachungaji Bethlehemu! Njooni kumtazama mototo Mzuri Mwana wa Mungu Amezaliwa. Baba amtuma awakomboe. Msiogope! Anatujia atufurahishe Njooni tumtukuze! Zienezwe popote sasa: Yesu mponya kaja Yesu mponya kaja. Usiku mtakatifu! Siku ya furaha Imetuangaza kimungu Tumeupewa ukombozi Kristo amefika Kristo amefika. Twnde Bethlehemu Tukaone Tulivyoambiwa na malaika. Tuyaonayo tutatangaza Na kutukuza kwa nyimbo Nzuri Haleluya! Kweli malaika Wametangaza Furaha kubwa kwa Wachungaji.

21. Watoto Njooni Bethlehemu

Watoto njooni, Bethlehemu, Njooni zizini kuona makuu Mungu aliyotutendea leo, Watoto waone furaha Kubwa. Twaona kitoto kizuri Hapa, wazee wamtazama, Wanafurahi? Wachungaji wote Wanangukia, Malaika wa mbingu Wanamwimbia. Pigeni magoti na Wachungaji! Wakubwa, wadogo Tumnyenyekee! Sasa popote patengenezwe, Na watu wote watapendezwa. Furahini! Tuimbe na sisi  kwa Furaha kuu Nyimbo za kumsifu Mwokozi Yesu! Watoka mbinguni Utuokoe, Waona uchungu sababu Yetu, Leo wazaliwa na mwana Kikiwa. Halafu wateswa, unatufia. Twapenda kukupa mioyo Yetu, Twataka kukutumikia vema. Takasa mioyo ikupendeze, Tupate kufika kwako Mbinguni.

22. Yesu Kitoto Kizuri

Yesu kitoto kizuri Umetujia watoto Utupe mioyo mizuri, Tuwe watoto wa mungu. Ee Mwanga toka Mbiguni Umetufikia sis, Tupate mwanga wa kweli, Tuunganishwe na Mungu. Mpenzi wangu Mtakatifu Umezaliwa duniani: Furaha iko kwa wote Kwa wakubwa na wadogo. Unibariki, ni mdogo, Moyo unisafishe, Ondoa taka ya roho, Upendo wetu uzidi!

23. Msifuni Mungu, Wakristo

Msifuni Mungu, Wakristo, Aliyetukuka, Atufungulia mbigu Kumtoa mwanaume:/ Atokaye kifuani Pa Mungu babaye, Alala sasa kitoto Kitupu, maskini: / Anyonya kwa mama yake, Maziwa chakula, Kwa kweli anatulisha Chakula cha mbigu. Ageuza hali yake, Avaa mwili wetu Na sisi anatuvika Uzima wa Mungu. Akawa mtumwa, na mimi Naitwa kibwana, Niwe nduguye na motto Wake Mungu Baba.;/

24. Ulimwenguni Pote

Ulimwenguni pote Asifiwe Mungu mkuu Amemtuma Mwokozi, Wakosaji wapone. Zamani wazee wale Wameona hamu kuu, Waondoshwe makosa Na kumpata Mwokozi. Abrahamu, Yakobo Na watu wa sayani Walimngojea sana, Sasa umetujia. Karibu mponya wangu Niondolee woga. Ujitengenezee Njia moyoni mwangu. Safisha nyumba yako Umfukuze Shetani, Yule nyoka wa kale. Nikutumikie wee!

25. Mungu ni wa Utukufu

Mungu ni wa utukufu Panapo mbinguni juu, Na kwao wampendezao Duniani raha-kuu. Sikieni nchi zote Huko mjini Bethlehemu: /: Kristo amezaliwa, Bwana wetu daima.:/ Watu na malaika wote Kuwa kama maskini. Akaacha enzi yake, Akavaa unyenyekevu Kristo amezaliwa…….. Asifiwe Mwana Mungu Na Mwokozi wa watu, Mleta mwanga na uzima Yesu mshinda kuzimu, Mfalme wa utengemano Huko mjini Bethlemu. Kristo amezaliwa,….

26. Nchi, Mbingu Furaha!

Nchi, mbigu furaha! Haleluya! Amekuja Mwokozi, Haleluya! Mwana wake Mungu Amekuja kwetu, Mwana amekuja kwetu. Toka shina la Yese, Haleluya! Tawi limechipuka, Haleluya! Mwana wake Mungu… Neno lake mwenyezi, Haleluya! Limekuja duniani, Haleluya! Mwana wake Mungu…..

27. Amezaliwa Mtoto

Amezaliwa motto Mjini Bethlehemu. Nimemchagua yeye, Niwe mali yake! Oye,oye, niwe mali yake! Nataka kuingia Pendoni mwake yee Na kumtolea moyo Hata vyangu vyote, Oye, oye, hata vyangu vyote. Kwa moyo wote safi Nataka kumpenda Shidani, furahani Hata kila wasaa. Oye, oye,hata kila wasaa. Unikubali hivyo, Naomba kabisa Nikuishie wewe, Leo na daima Oye, oye, leo na daima!

28. Amkeni Upesi

Amkeni upesi Wachunga kondoo! Malaika washuka, Habari watupa: Furaha karibu, Mwokozi aja! Wachungaji njooni, Tumtafuteni! Akiwa zizini Pengine filimbi Furaha karibu… Wachungaji hima Washika njia. Pamoja wamwona Mamaye, babaye. Furaha karibu….. Wamjua upesi Mototo wa mbingu. Wapiga magati Kumwimbia nyimbo. Furaha karibu…

29. Siku ya Furaha Popote

Siku ya furaha popote, Sauti za kusifu zavuma! Duniani, nyumbani Nyimbo za furaha kuu: Siku za furaha popote, Sauti za kusifu zavuma! Azaliwa Mesiya kwetu Duniani: Tulio wa gizani, Tuwe wa mwanga. Siku ya furaha popote…… Siku ya furaha popote, Sauti za kusifu zavuma! Duniani, nyumbani Nyimbo za furaha kuu: Siku ya furaha popote, Sauti za kusifu zavuma!

30. Mpige Mbio, Wachungaji

Mpige mbio, wachungaji Mpige mbio wote, Chukueni na filimbi Na zumari pia. Mpige mbio wote, Mpige mbio wote Bethlehemu Kwenye hori Waliomo ng’ombe. Mumtazama mototo mzuri Aliyezaliwa, Na wazazi wake motto Wako huko naye Ni Yosefu baba Na Maria mama, Mwanamwili mzuri sana Kama malaika juu. Hebu njooni,ee jamani Mlete nguo nzuri! Tumlazeni motto wetu Kwa uzuri wote! Twakubembeleza Wewe motto lala! Lala Yesu mpenzi wetu Twakubembeleza.

31. Malaika Njooni Toka juu!

Malaika njooni toka juu! Oye,oye, tazama, tazama kitoto. Kwa sauti kuu mwimbieni! Oye,oye Tazam, tazama kitoto. Kwa vinanda na vinubi. Haleluya! Haleluya! Nyimbo za Yesu na Maria! Tungeni nyimbo tamu mno Oye,oye, Tazama, tazama kitoto, Kupita ndege wa aanga. Haleluya! Haleluya! Nyimbo za Yesu na Maria. Imbeni, pigeni panda. Haleluya! Haleluya! Nyimbo za Yesu na Maria! Utamu wa nyimbo zenu Oye, oye, Tazama, tazama kitoto, Umbembeleze, alale. Haleluya! Haleluya! Nyimbo za Yesu na Maria. Watu watengemane, Oye, oye, Tazama, tazama kitoto, Na Mungu tumpe Shukrani! Haleluya! Haleluya! Nyimbo za Yesu na Maria.

32. Kitoto Mpenzi Lala Wee

  Kitoto mpenzi lala wee, Motto wa mbiguni! Malaika wakupepea Ulale kwa raha. Nasi maskini wachunga Tunakubembeleza wee. Ulale, lala Kitoto wee, ulale. Maria kwa upendo mkuu Amlaza vizuri. Yosefu vizuri. Yesefu amekaa kimya Ili asimwamshe. Na wanyama wa nyumbani Wamenyamaza kabisa: Ulale,lala Kitoto wee, ulale. Utakapokua Yesu, Watakuumiza. Kilimani pa Golgota, Utasubilishwa. Kwa hiyo sasa lala tu! Kwa raha na utulivu! Ulale, lala. Kitoto wee, ulale

33. Niende na Wachungaji

Niende na wachungaji Nimtazame mponya wangu, Kazaliwa duniani Kwa kunipenda mimi. Nimwimbie na malaika, Niusifu utukufu. Anautengemaza Kila moyo unipende. Nikawaze na Maria Jambo hili la ajabu: Acha mwili mzuri, Achukua wa kimtu. Nimpelekee vipaji Na watambuzi wa nyota, Na nimpe maji yangu, Hata uzima nimpe. Nakupenda, u Mwokozi, Nikumbuke siku hii. Uje mwangu moyoni, Uufanye kikao.

34. Wakristo Furahini

Wakristo furahini, Furahini sana! Mwaipigiwa leo Mbiu yenu njema! Malaika wanaimba Huko juu mbinguni, /:wanaimba vizuri Sauti ya kushangaa!:/ Hivi wanavyoimba: Furahini nyote! Acheni kuogopa, Tazama nyote Kwani amezaliwa Mwokozi wa pekee: /: ni Bwana Yesu Kristo, Mwana Mungu wetu!:/ Shangilieni nyote Na kusikiliza. Wapigieni nyote Mbiu na sauti kuu. Mungu katupa sote Motto wa mbinguni, /: kwa kutupenda sisi Amekuja kwetu. :/

35. Tazama, Nawatangazia

Tazama nawatangazia, Nawatangazia, Nawatangazia, Shangwe kubwa, Shangwe kubwa, Shangwe kubwa, Shangwe kubwa. Shangwe, Shangwe kubwa inayokuja, Kwa watu wot, makoo yote; Inayokuja, inayokuja Amezaliwa leo Bwana Mwokozi,ndiye Kristo Yesu, Bwana wa mjini mwa Daudi, Wa mjini mwa Daudi!

36. Mwema, Mwema,Mwema

Mwema, mwema, Mwema ni Bwana mbinguni, Na utengemano Kwa watu wanaompendeza, Kwa watu wanaompendeza. Mwema ni Bwana mbinguni. Mwema ni Bwana mbinguni, Nchi itengemane, Watu wapendezwe Wote wakampendeze Bwana. Mwema,mwema,mwema Ni Bwana mbinguni Na utengemano Kwa watu wanaompendeza Kwa watu wanaompendeza! 37. Sote Tufurahi K:  Sote tufurahi, W: Habari ni njema K:  Njoni nyote wahi, W: Tupate uzima. Sasa yametimia Yaliyotabiriwa. Mwokozi kazaliwa. K:  Kule Bethlehemu W: Yesu kazaliwa K:  Mama Mariamu W: Alivyoambiwa. Sasa yametimia…. K:  Kumbe, huyo Mwana W: kazaliwa horini K:  Huyo Yesu Mwana W: akawa shidani. Sasa yametimia… K: Mwana atiiye W: ni Bwana shujaa, K:  Kwake tuwe wana, W: ni Mponya dunia. Sasa yametimia…. K:  Jeshi la mbinguni W: katoa Injili. K:  Watu walishoni, W:  kaona ni kweli. Sasa yametimia… K:  Mungu yupo nasi W: katika dunia. K:  Pendo kwa waasi, W: katoa kwa nia. Sasa yametimia….. K:  Raha na tushik...

37. Sote Tufurahi

K:  Sote tufurahi, W: Habari ni njema K:  Njoni nyote wahi, W: Tupate uzima. Sasa yametimia Yaliyotabiriwa. Mwokozi kazaliwa. K:  Kule Bethlehemu W: Yesu kazaliwa K:  Mama Mariamu W: Alivyoambiwa. Sasa yametimia…. K:  Kumbe, huyo Mwana W: kazaliwa horini K:  Huyo Yesu Mwana W: akawa shidani. Sasa yametimia… K: Mwana atiiye W: ni Bwana shujaa, K:  Kwake tuwe wana, W: ni Mponya dunia. Sasa yametimia…. K:  Jeshi la mbinguni W: katoa Injili. K:  Watu walishoni, W:  kaona ni kweli. Sasa yametimia… K:  Mungu yupo nasi W: katika dunia. K:  Pendo kwa waasi, W: katoa kwa nia. Sasa yametimia….. K:  Raha na tushike, W: tunaye Masihi K:  Haya twende kwake W: sauti zasihi. Sasa yametimia….. K: Wote wenye Mwana W: wanao uzima. K: Yeye ndiye Bwana, W: atoa karama. Sasa yametimia….. K:  Nyota yatunuka W: shinani mwa Yese K:  Bwana atukuka, W: akatutakase. Sasa yametimia... K: Sasa, ndugu nyote, W: tangaza neema. K:  Wa...

38. Sauti Imetoka Mbinguni

K: /: Sauti imetoka Mbinguni; W:   Sauti imetoka Mbinguni. :/ K: /: Ahubiri malaika Wake Mungu. :/ W:   Ahubiri malaika Wake Mungu. :/ K: /: Ninyi watu acha Kuogopa: W:   Ninyi watu acha Kuogopa. :/ K: /: Nawaletea habari Furahini: W:   Nawaletea habari Furahini.:/ K: /: Leo amezaliwa Mwokozi; W:   Leo amezaliwa Mwokozi; / K: /:Kazaliwa Kristo; Ni Mwokozi wenu; W: Kazliwa Kristo; Mwokozi wenu. :/ K: /: Mtamwona huyo Kalazwa,horini; W:  Mtamwona huyo Kalazwa, horini. :/ K: /: Mtamwona Amevikwa nguo; W:  Mtamwona Amevikwa nguo.:/ K: /: Nanyi makundi, Huko mbinguni; W:   Nanyi makundi, Huko mbinguni. :/ K: Saidia kumshukuru Mungu wetu; W: Saidia kushukuru Mungu wetu. :/ K: Utukufu wa Mungu Mbinguni; W: Utukufu wa Mungu Mbinguni. :/ K: /: Kawapa watu Amani duniani; W: Kawapa watu amani Duniani. :/ K: /: Hakika Mungu Ametuona; W:   Hakika Mungu Ametuona. :/ K: /:Tufurahi, Tumfurahie Mwokozi; W:  Tufurahi, tu...

39. Tumezaliwa Mtoto

K: Tumezaliwa motto, Tumezaliwa motto. Ni Bwana Yesu, Atakayewachunga Kondoo. W: Amezaliwa motto. Asante, Bwana Mungu. /:   Ulivyoona kondoo Wako,huku chini ya Mbingu, Hawana mchungaji. :/ K: Wewe Mama Mariamu, Wewe Mama Mariamu, Utaziona huzuni nyingi Atakapotimiza sheria. W:  Wewe Mama Mariumu, Na umshukuru Mungu, /: Alivyoona kondoo Wake, huku chini ya Mbingu, Hawana mchungaji. :/ K:  Ni furaha yetu kubwa, Ni furaha yetu kubwa, Tukitumiwa Mwokozi Yesu Ili atupiganie vita. W:  Nifuraha yetu kubwa, Na tumshukuru Mungu. /: Alivyoona kondoo Wake, huku chini ya Mbingu, Hawana mchungaji. :/

40. Tushangilie Sote

  K:  Tushangilie sote W:  Kila mtu. K:  Mwana wa Mungu Akaja W: Hata kwetu K:  Tumjue Mungu Baba W:  Wa huruma. K:  Usiku wa manane W:  Shangwe kubwa. K:  Alipozaliwa Kristo W: Awe Mfalme. K:  Pale katika mji W:  Wa Daudi. K:  Kwenye kondoo hata Ng’ombe W: Bethlehemu. K:  Na akaitwa kwa jina W:  La ajabu K:  Nalo Yesu Mwokozi W: Mungu nasi K: Hakika ni Mwokozi W:  Mwenye  enzi. K: Tupatiwe uzima W:  Wa milele K:  Na kumtumikia Daima W: Siku zote. K:  Maana kwake sasa Tumemwona W:  Mungu wetu K:  Na hiyo hata Roho W:  Mtakativu K:  Njoni kwa hiyo Tumsifu W:  Bila mwisho

41. Tumepata Mwokozi

K:   Tumepata Mwokozi sasa Bwana Yesu, W:   Ee, tumepata Mwokozi sasa. K:    Duniani hatuna mtu Hata mmoja. W:    Ee, duniani hatuna Mtu. K:     Tutafute msaada wapi Huko chini! W:     Ee, tutafute msaada Wapi? K:      Peke yetu tungepotea. Peke yetu. W:      Ee, peke yetu Tungepotea. K:       Yuko Yesu peke Yake tu, yuko Yesu W:       Ee, yoko Yesu Peke yake tu. K:       Asema, Nakufia Wewe mwanadamu, W:       Ee, asema, Nakufia Wewe. K:        Katumwagia damu Yake msalabani. W:        Ee, katumwagia Damu yake. K:        Katulipia dhambi Sisi wakosaji. W:       Ee, katulipia dhambi Sisi. K:       Katupatanisha na Mungu, Haleluya. W:  Ee kutupatanisha na Mungu. K:  Kwa sababu hiyo ni Wake, mali yake. W...

42. Ilitoka Nuru Kuu

Ilitoka nuru kuu, Kuliko nuru zote; Na huo wimbo wa juu Wapiti nyimbo zote; Ndiyo habari tukufu, Ya Kristo wa utukufu, Awajia wapole; Ni Mungu pamoja na sisi Imanueli. Mwaka huandama Mwaka, Wimbo huo na uimbwe; Wapenda kukumbuka, Mzee na wanawe, Ndiyo habari tukufu, Ya Kristo wa utukufu, Awajia wapole; Ni Mungu pamoja na sisi, Imanueli. Twafurahi siku hii Ijavyo kila mwaka; Nasi tufanye bidii Huku tukikumbuka, Ndiyo habari tukufu, Ya Kristo wa utukufu, Awajia wapole; Ni Mungu pamoja na sisi Imanueli.

43. Yesu Ulale

K:   Yesu, ulale, W:   Haleluya. K:    Tulia, Mwana, W:   Haleluya. K:    Tulia, Mwana, W:    Haleluya. K:    Mwana wa Maria, W:    Haleluya K:    Mwana wa Daudi, W:   Haleluya. K:    Shina la Yese, W:   Haleluya K:    Haleluya W:   Haleluya Mtoto. Ee, Mwema tu, Kila anayekuamini, Utamgawia amani tu. K:  Lala, Ee Yesu, W: Haleluya. K:  Lala, Ee Yesu W:  Haleluya. K:   Ufumbue macho, W:   Haleluya. K:    Mzao wa Ibrahimu, W:   Haleluya. K:    Mwana wa Isaka, W:   Haleluya, K:    Mrithi wa Yakobo, W:   Haleluya. K:    Haleluya. W:   Haleluya. Mtoto Ee....

44. Mjini Mwake Daudi

Mjini mwake Daudi Bandani mwa mifugo Mtoto alizaliwa Na mamaye maskini Mariumu ni mama Yesu mwanawe mwema. Yesu akawa mbinguni Akatoka enzini Hakukaribishwa chini Akalazwa horini Akaja kimaskini Kuketi duniani. Siku za ujana wake Akimheshimu mama Na kumtii katika yote Kama alivyosema. Kila mwana na awe Mtii kama yeye. Amekuwa hata sasa Kielelezo chetu Alikuwa na unyonge Kama unyonge wetu Kucheka na kulia Ni kama sisi sote. Tutamwona waziwazi Ndiyo ahadi yake Sasa aketi mbinguni Katika enzi yake Sote na tumwandame Kwani ni Mfalme wetu. Tumwona Yeye tena! Si katika kibanda, Ila juu: nasi sote Kwake tutakutana, Hivyo tutasimama Mbele yake daima.

45. Bwana Yesu Amezaliwa

K:  Bwana Yesu, W: Ee, amezaliwa. K:  Wachungaji, W:  Ee wamsujudia. K:  Na mamajusi, W: Ee wamsujudia. K:  /: Na sisi sote, W: Ee, tumsujudie. :/ K:  Amefika, W: Ee, atukomboe. K:  Atimiza, W:   Ee, hadi ya kale. K:    Aliahidi, W:   Ee, yeye peke yake K:    /: Na sisi sote W:   Ee, tumsujudie. :/ K:   Isaya naye, W:  Ee, alitangaza. K:   Kwamba Mwokozi, W:  Ee, atazaliwa. K:   Tangazo lake, W:  Ee, limetimia. K:   /:  Na sisi sote, W:  Ee, tumsujudie. :/ K:  Malaika, W: Ee, waona furaha. K:  Wamwabudu, W: Ee, na kumwimbia. K:  Na nyimbo zao, W:  Ee, zimesikiwa. K:  /: Na sisi sote, W: Ee, tumsujudie. :/ K:  Haleluya, W: Ee, furahi wote, K:  Na tumpokee, W: Ee, mioyoni mwetu. K:  Akae nasi, W: Ee maishani mwetu. K:  /: Na sisi sote, W:  Ee, tumsujudie. :/

46. Twendeni Tumshukuru

Twendeni tumshukuru Na kumwimbia Mungu, Aliyetupa roho Na nguvu mpaka leo. Twaenda na kukua Miaka yetu yote, Hivyo mwaka kwa mwaka Twafikia uzee. Twaona shida nyingi, Uchungu na mateso Na vita na misiba Katika ulimwengu. Kuhangaika kwetu Siku zote ni bure Asipotushikiza Yeye atulindaye, Na kama mama mwema Anavyomlinda mtoto Katika shida zote, Asipotee njia. Hivyo na Mungu wetu Hulinda watu wake, Huwakingia shida, Huzuni na misiba. Huruma zako ni mpya Kila panapokucha, Hizo zinakomesha Uchungu wa mioyo. Utabariki sote Katika njia zetu, Wakubwa kwa wadogo Wakalishe mwangani. U baba wa wakiwa, U mshauri wa wajinga, U mponya wa wagonjwa, U msaada wa maskini. Na mwisho twakuomba; Utupe roho yako, Atufundishe hapa, Atuongoza kwako. Wewe mwenye uzima Utupe haya yote Sisi wakristo wako! Kwani twakungojea!

47. Anza Siku Yako Hii

Anza siku yako hii Kwa jila la Yesu; Mwombe akujalie, Usimame naye. Kazi zako zote wee Atazibariki. Na tena ulalapo, Atakuwa kwako. Asubuhi mapema Umwombe Mwokozi, Akusaidie yee Shidani popote. Atasimama kwako Siku kuchwa pia, Na kumshinda Shetani Akikujaribu. Yesu akiwa nawe, Waacha maadui, Usiogope hila Zao zote mbaya, Umtegemee Yesu, Shika mkono wake; Mtegemee Mwokozi, Yeye atashinda. Mambo yangu na shida Nazikuwekea Kama unavyopenda, Zimalize zote. Kazi yangu nianze Kwa jina la Yesu Nakuomba: Njoo kwangu, Unisaidie!

48. Yesu Mponya tu Hapa

Yesu mponya tu hapa, Moyo watulia, Mawazo yetu yote Uyavute kwako. Mwanga wa neno lako, Utuangaze wote, Tuwe na mwangazo. Kaa karibu na sisi, Tunakutamani, Mfunzi wetu ni wewe, Sisi wanafunzi. Nenolo lina nguvu, Litatufanya wapya, Laongoza vema. Tuna furaha kubwa, Tunakungojea. Wewe u mwamba wetu Tutegemeao. Bwana tunakushika Mpaka tunapofika Uzimani kwako.

49. Nakutegemea Yesu

Nakutegemea Yesu, Yesu peke yako tu. Wewe u mkombozi wangu Unitulizaye. Nakutegemea Yesu, Kwani u mkombozi Ukinifia. Ndipo nikakupenda sana, Wala sikuachi! Wewe mfalme mkubwa Sana Unaondoa dhambi. Wanionea huruma, Huna madanganyo. Nakutegemea Yesu,… Wewe umechunga Kondoo, Wamtangulia mwanga. Nakungoja mwongozaji Nisipotee njia. Nakutegemea Yesu,….. Wanichukulia mzigo, Sianguki majini. Natambua wanipenda, Huniachi pekee. Nakutegemea Yesu,…

50. Twapenda Ukaapo

Twapenda ukaapo Bwana wetu enzini, Furaha zako wewe Zinazipita zote. Palipo pa kuomba Wajapo watu wako Na wewe Bwana upo, Uwakubali wote. Twapenda neno lako, Habari za wokovu, Za nguvu za kushinda, Za shangwe za mbinguni. Twapenda nyimbo zako, Tunaziimba hapa, Mpaka tutaziimba Pamoja na malaika. Utujalie Yesu, Tuzidi kukupenda, Tuone uso wako Utakavyotakata.

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu

Yesu ndiye kiongozi Wangu, Kumfuata yeye ni furaha, Ajuaye kuongoza vema, Anilinda, nisione shida, Analeta raha moyoni. Bwana yesu Akiniogoza, Nitapita pori na misitu, Nitavuka mito na bahari Kwa furaha, Kwani nina njia Yakufika mjini kwa Mungu. Nikilala Yesu anilinda, Anitunza yeye siku zote. Hata nikifika njia panda, Nikiona shaka, aonyesha Njia ya kufika kwake. Siku zote namfuata yeye, Sitaona kiu wala njaa; Anitunza kwa rehema Nyingi; Nitaweka mikononi mwake Moyo wangu, auokoe.

52. Jina Lake Yesu Tamu

Jina lake Yesu tamu; Tukilisikia Hutupoza, tena hamu Hutuondolea. Roho iliyoumia Kwalo hutibika, Chakula, njaa pia; Raha, tukichoka. Jina hili ni msingi, Ngao, ngome, mwamba, Kwa hili Napata wingi Kwangu ni akiba. Yesu, Mchunga, Rafiki, Mwalimu, kuhani, Mwanzo, Mwisho, njia, Haki, Uzima kifoni. Moyo wangu hauwezi Kukusifu kweli, Ila sifa zangu hizi, Bwana zikubali. Na utakaponiita, Kuja kwako Bwana, Huko kwako sitaacha Kukusifu sana.

53. Tumshukuru, Tumsifu

K:  Tumshukuru, tumsifu Mungu kwani ni mwema. W:  Huruma yake ipo, Mchana na usiku. K:  Tangaza jina lake, Mungu wetu wa kweli. W:   Huruma yake……. K:  Kajaza maajabu, Mbinguni duniani. W:  Huruma yake…….. K:  Kwa uwezo wake Mkuu, Ameviumba vyote. W:  Huruma yake…….. K:  Aliongoza watu, Ugenini zamani. W:  Huruma yake….. K:  Maskini katupa, Hapa ulimwenguni. W:  Huruma yake……. K:  Anawalisha watu, hata Wanyama pia. W:  Huruama yake……. K:  Na tumwimbie Mungu, Kwani yeye ni mwema. W:  Huruma yake….

54. Yesu, u Nyota Kubwa

Yesu, u nyota kubwa, Itokayo wangu wapenda Kukutumikia leo. Ukubali vipaji Niviletavyo mimi. Ninaleta dhahabu, Ndio kukutegemea, Nalo ni paji lako, Ulilonipa mwenyewe; Nikushike kwa kweli Hata majaribu. Nao uvumba wangu Ni maombi yangu mimi; Midomo na mioyo Isikome kuyatoa. Uyakubali haya Kuwa uvumba mzuri. Nayo majuto yangu Ndiyo manemane yako; Kwani hunipokea, Nikikujutia kweli. Nasema kwa furaha: Watwaa matunzo yangu!

55. Mmoja Ndiye

Mmoja ndiye Tumpendaye Aliyetoa mwili wake Akikubali mateso. Twakupa mioyo yetu Mwokozi uliyetufia, Twapenda kuwa wako tu. Bwana tukubali! Ututengeneze sisi wako. Nuru yako itung’aze Tusipotee gizani, Sisi hatukukuita, Ila umetuita wewe, Huruma yako ni kubwa. Nguvu zetu hazitoshi, Kukufanyia kazi njema Usipotutia nguvu. Shida yetu sisi Ndio ulegevu, uondoe; Nia zetu zigeuzwe Tufanye kazi kwa bidii. Yesu, wewe umesema: ‘’Watenda kazi ni wachache Kweny mavuno ya Bwana’’ Twaomba: Tutume nasi, Tualike wageni wengi, Nyumba ya Bwana ijae. Heri watu wale Uliochagua kuja kwako Kwenye raha na furaha, Milele hata milele. Uwahurumie watu Walio mbali na wokovu Wanaoshikwa nagiza. Hawajasikia bado Utume mwema wa wakovu Tunaopewa na Mungu. Jua la uzima Liche hata kwao. Njoo Mwokozi! Tangulia! Twafuata, Ukifungua milango. Tunataka kutangaza Habari ya upendo wako, Ya moyo wako wa kweli Tutawaonyesha watu Msalaba wako siku zote, Mpaka washindwe mioyoni, Kwani neno lako Lina nguvu kubwa ya Kushinda. Mzi...

56. Mmoja ni Mfalme

Mmoja ni mfalme shujaa, Ni mshindaji! Enyi adui, kimbieni tu! Nawe Sayuni uone furaha Ukapumzishe kabisa moyo: Uzima, utengemano, furaha Ndizo Mwokozi Atakazokupa. Twende kuonja maji ya uzima Tunayopewa na Bwana Yesu, Aliyesema ‘’Njooni kwangu wote, Nitapumzisha mioyo yenu’’ Nyweni, wapenzi, katika Kisima Chenye wokovu wa wenye Huzuni. Mfalme wa mbigu Ataka kuwapa Kilemba kizuri cha urembo, Awawekea viti vya milele, Heshima hiyo ni ya kushinda. Vumilieni tabu na shida: Yesu mwenyewe ni tuzo la Vita. Nguvu, ujuzi, heshima Na sifa Ni zake Mungu na Mwamwa Wake. Name nataka kufika Mbinguni! Nifunguliwe  mafungo yangu! Mwenye upendo atanisikia. Wenye uzima wanamsifu Mungu.

57. Nani Mpenzi Wangu Mkuu?

Nani mpenzi wangu Mkuu? Nani ninayemsifu? Nani ninayemjua? Nani ninayempenda? /: Ndiye Yesu Mwokozi.:/ Nani nimtegemee, Anipaye moyo mkuu? Nani aondoaye Makosa, shida zangu? /: Ndiye Yesu Mwokozi. :/ Nani anayenipa Nguvu nyingi za roho? Nani anifanyaye Mwenye haki kwa Mungu. /: Ndiye Yesu Mwokozi. :/ Nani azishindaye Hata nguvu za kufa? Nani anipeleke Baadaye kwake Mungu? /: Ndiye Yesu Mwokozi.:/

58. Jina Moja ni Kubwa sana

Jina moja ni kubwa sasa; Ni jina lako Bwanangu! Nasifu jina hili lako, Yesu Kristo u Mwokozi. Li tamu kwangu jina hili, Jina lingine silijui. Naliandika jina hili Rohoni mwangu kabisa. Silisahau siku zote, Halifutiki moyoni. Li tamu kwangu jina hili, Jina lingene sitafuti. Jina hili ni jua langu Lawaka ndani ya roho. Lanipa na utengemano, Lafuta makosa yote. Li tamu kwangu jina hili, Jina linguine sifahamu. Jina hili ni boma langu, Upanga wangu vitani, Ni ngao yangu na silaha, Lamshinda hata Shetani. Li tamu kwangu jina hili, Jina linguine silitaki. Jina hili lanipa nguvu, Niweza kwenda kwa haki. Ujuzi wote umo humo Katika jina la Yesu. Li tamu kwangu jina hili, Jina linguine sitamani. Ee Yesu, jina lako ndilo Furaha yangu nikifa. Ni cheti cha kuingilia Mbinguni kwa Bwana Mungu Ndipo nitalisifu sana, Jina linguine silijui.

59. Kazi ni Yako Bwanangu

Kazi ni yako Bwanangu tunayoifanya; Hakuna ayeweza Kuvunja kazi hii. Ni kama punje ya mbegu ikiwa ndani ya mchanga, inakufa kwa kuoza; na hapo yabadilika, inaota, yakua na kuzaa. Yesu umeteswa kwanza, Halafu umepaa. Nao wakufuatao Wanateswa vivyo. Twaomba tusaidie nasi tushike njia hii, kwa kufa kwako na sisi tunatoka kaburini. Tuongoze, tufike mbinguni. Bwana wewe umekufa kwa ajili yetu Ukaweka ufufuo ulipofufuka. Twaomba: Tuma motume, wajulishe jina lako mpaka mwisho wa dunia. Utakubali na sisi kwa kazi hii,tutume, twakutii!

60. Ufalme wa Mungu

Ufalme wa Mungu uenee popote! Nguvu yako iokoe wakaao gizani. Uondoe woga wote, ukawape watu uzima, ufalme wa Mungu. Ushinde upesi! Uharibu ufalme wa shetani duniani, ndiye mfalme wa giza. Nawe utamshinda yeye, Kwani una nguvu ya Mungu Ushinde upesi! U Shujaa wa Mungu! Kwa rehema ya Bwana urudishe watu wako’ wapendane kwa moyo, wawe raia wako pote. Ndipo utatukuzwa sana! U shujaa wa Mungu! Duniani popote jina lako livume nguvu zako zi sifiwe na makabila yote, uliowatengemaza, mpaka utakapo tawala duniani popote! Shikeni amri hii: Tangazeni popote kwa makabila yoyote neno lenye furaha, wapate kuokolewa. Yesu alivyotuagiza. Shikeni amri hii! Sifuni rehema Ya kuokoa watu! Tukimtumikia Bwana. azibariki kazi zote za mikono yetu; Amani kuu iwe kwetu. Sifuni rehema!

61. Sifuni Nyote Huruma

Sifuni nyote huruma ya Mungu, Kwa nyimbo nzuri, Umati wa Yesu! Atualika furahini: /:Msifuni Bwana kwa neema yake:/ Yeye ni Mfalme Anaye tawala; Viumbe vyote Vinamtumikia, Hata malaika, Wamwabudu, /:wanambwimbia kwa sauti nzuri:/ Enyi amataifa, Hofu iacheni! Njooni kwa Yesu, Mchunga kondoo mwema. Sikilizeni Neno lake: /:Atukomboa kwa kufa kwake:/ Awapa watu chakula chochote, Atushibisha kama baba mzuri, Aleta jua hata mvua, /:Atubariki kwa wema wake:/ Sifuni nyote huruma ya Mungu, Kwa nyimbo nzuri, Umati wa Yesu! Sasa  huzuni twaishinda: /:Msifuni Bwana neema yake!:/

62. Uamke Kwetu Tena Roho

Uamke kwetu tena Roho Wa mashahidi wale kwanza, Waliolesha siku zote, Waliomshinda Yule adui, Wakihubiri Neno la Yesu Kwa watu wa ulimwengu wote. Uwashe moto wa Upendo, Uendelee pote kuwaka. Peleka watu mavunnoni, Wanao fanya kazi kwa bidii. Bwana mwenye mavuno, Tazama: Watenda kazi yako ni haba. Mwanao ametuagiza Kuomba hivi kwa Jina lake, Na sisi wanafunzi wake, Twashika Neno Lake kwa bidii. Twaomba hivi kwa moyo wote. Ee Bwana usikie, ufanye! Utume watu wengi sana, Walitangaze Neno kwa nguvu. Tusaidie, tuokoe; Ufalme wa Shetani uishe. Usimamishe, Bwana wa mbinguni, Ufalme wako Ulimwenguni! Utume mwema na uende Mahali popote huku nchini. Wadiini zote waingie, Kundini mwako mwa wateule. Amsha nao Wana wa  ahadi Na wa Imani zote wakutii.

63. Yesu Mfalme Utiishe

Yesu, mfalme, utiishe Upesi ulimwengu wote, Viumbe vyote vikutii. Ubariki Neno lako, Utoe Roho za uzima, Uamshe waliolala. Bwana usikie Tunavyokuomba. Amen, Amen! Tutaimba Haleluya Na nyimbo za kukusifu.

64. Yesu Mwokozi

Yesu mwokozi Mwenye nguvu zote, Wewe mwana wa Mungu Nitakupenda, nitakusifu Uliye mpenzi wangu mkuu Uzuri wote Wa nchi na milima unatufurahisha. Yesu nimzuri kupita hiyo anatufariji sisi. Jua na mwezi Hata nyota zote zinang’aa mbinguni. Yesu ashinda uzuri huo, Ang’aza watu mioyo. Uzuri wote hapa na mbinguni Ni mfano wa Mwokozi Tumpende Yeye wa utukufu. Aliyetupenda kwanza.

65. Yesu ni Mponya

Yesu ni Mponya, Aleta furaha! Mwanzo na mwisho Wa vyote ndiye. Mwana Adamu Na Mungu wa kweli Ametujia atubariki. Mbingu, dunia, Toeni habari: Yesu ni Mponya, Aleta furaha! Yesu ni Mponya Aleta wokovu! Sikilizeni habari njema! Sisi tulipomwacha Mungu wetu Akaturudisha tena kwake. Ametufanya watoto Wa Mungu. Yesu ni Mponya Aleta wokovu. Yesu ni Mponya, Aleta uzima Kamba za kufa zimekatika. Mwana wa Mungu Kumshinda Shetani, Awakomboe watumwa wake, Amewapata, kawapa uhuru. Yesu ni Mponya, Aleta uzima Yesu ni Mponya, Mchungaji wa kweli, Amaye lisha vizuri kondoo. Wote walio mbali awaita, Awarudishe kundini mwake. Awakomboa kondoo kuani: Yesu ni Mponya Mchungaji wa kweli. Yesu ni Mponya Na mfalme wa enzi! Mbingu zimsifu na watu wamtii Anageuza mioyo ya watu, Hata na sisi tumpe yetu, Kwani apenda kutupa uzima. Yesu ni Mponya Na Mfalme wa enzi! Yesu ni Mponya Na mwenye upendo! Anatupenda Kwa moyo wote. Yeye mwenyewe. Upendo wa kweli, Aliyekufa kwa kutupenda. Nasi tumpendaye kwa nguvu ya roho! ...

66. Mfalme ni Yesu Pekee

Mfalme ni Yesu pekee, Wote wanamwangukia, Watawalishwa na Mungu, Ndimi zote ziungame Yesu ni Mfalme wa pekee, Atukuzwe popote. Maflme mkubwa, Watu wako Wakutii, wanakusifu. Yesu apita wafalme, Yeye ndiye mkubwa sana, Apenda kuwakomboa, Kwani ndiye Mwokozi. Enyi watu mpeni mioyo, Mnaohuzunika njooni, Wakiwa semeni naye, Kwani vyote aviweza Awagawia uzima Wanaomngoja yeye. Kama wataka uzima, Nenda kwake, acha soni, Yeye anakungoja. Amejitoa mwenyewe, Wewe upate kurithi Mbingu ni yako sasa. Nimsifuje Yesu Kristo Mimi vumbi, mimi jivu? Nasema: nitamtangaza Kristo Yesu ndiye Bwana! Na tumpende, Tumheshimu Sifa zote zampasa.

67. Nyesha Mvua

Nyesha mvua, nyesha mvua, Wewe Roho wa Baba, Nchi kavu ikanyweshwe, Insifu Mungu wetu! Vuma sana, vuma sana Roho mwenye uzima, Tulio na usingizi Utuamshe kwa mkono! Toa mwanga, toa mwanga, Roho kwani unang’aa Wewe ushinde usiku Tusikae na giza. Sikiliza, sikiliza, Wewe Mflme wa mbingu! Tuma Roho wako kwetu, Kote kuwe na upya!

68. Nitakutukuza

Nitakutukuza, Nakuimbia /: wewe uzima wangu, Kingojeo changu!:/ Umeniokoa kwa mkono wako, /:nalifuata njia ya upotevuni:/ Wote wakujue upole wako, /:wakufuate Yesu ninayekupenda:/ Utume mitume waende kote, /:kwa nguvu yako Bwana wafu wafufuke:/ Huku chini kote, Dunia nzima /: lifanywe kundi moja, wewe Mchunga wao!:/

69. Wito Waja

Wito waja, kwa nchi zote Wapi washindi wa Yesu Watakaomfuata kweli? Sisi tujitie kwake! Mkubwa nani? Tushikane Naye mfalme,  tupatane, tumfuate! Ana ufalme tangu kale, Nchi hata mbingu ni zake. Atuelekeze juu kwake, Hatahukumiwa tena. Mkubwa nani? … Tutangaze utume mwema Kwa makabila ya kwetu, Na tuseme pasipo woga Tuyaonayo kwa Yesu. Mkubwa nani? … Haya jamaa tuwe tayari Sisi watumishi wake, Yeye ni Mfalme wa majeshi, Miili na mioyo ni yake Mkubwa nani? …

70. Twende Vitani

Twende vitani vitakatifu, Zikitujia, shida na taabu. Ngurumo zivume kutia woga. Mwiteni Mwokozi! Yesu mwanga. Ingawa giza lawafunika, Na rah yenu ikizimika, Na nguvu za mwovu Hazina mpaka. Mwiteni Mwokozi… Shetani aje, akijaribu Kuvunja kazi na kuharibu Hila zake zote na zitakwisha. Mwiteni Mwokozi …

71. Wajibu Mwema Watoka Kwako

K:   Wajibu mwema watoka kwako, Bwana mwenye utukufu. Neno jema ndilo jina lako. W:  /:Yesu ni mwanzo wa kazi shamabni, tena ni Bwana, wa nguvu kwa utume wetu:/ K:   Watendakazi mwako shambani, Uwape matumaini. Nazo nguvu wakiwa kazini. W:   /: Watende yote kwa uaminifu, Wawe makini, Huduma isiharibike. :/ K:  Wapate heri kuyasikia uliyo yaagizia. Waje nao kutuhubiria. W:  /: Tena kazini Wakaelexee Neno Kwa wazi, na kweli Ya uzima wako. :/ K:   Wajihadhari wawe Na hamu, Kushika na kufahamu. Jina lako lika warehemu. W:   Ni wachungaji, Waju hilo tu Si watawala. Bwana, ujifunue kwao.:/ K:   Unawatuma Katika kundi, Kwa bidii na juhudi. Nasi kwao Tuwe mashahidi. W:   /: Ushangiliwe Kwa neema yako, Na kundi lako Lijue lina viongozi:/

72. Tumesikia Mbiu

Tumesikia mbiu: Yesu, loo! Aponya; Itangazeni kote, Yesu loo! Aponya. Tiini amri hiyo: Nchini na baharini, Enezeni mbiu hii: Yesu loo! Aponya. Imbeni na vitani: Yesu loo! Aponya; Kwa nguvu ya Mkombozi, Yesu loo! aponya. Imbeni wenye shida, Unapo umwa moyo, Na kaburini imba: Yesu, loo! Aponya. Mawimbini ienee: Yesu, loo! Aponya Wenye dhambi jueni: Yesu, loo! Aponya Visiwa na viimbe, Vilindi itikeni, Nchi shangilieni: Yesu, loo! Aponya. Upepo utangaze: Yesu, loo! Aponya; Mataifa yashangaa; Yesu loo! Aponya. Milimani, bondeni, Sauti isikike Y wimbo wa washindi: Yesu loo! Aponya.

73. Ni Ujumbe wa Bwana

Ni ujumbe wa Bwana Haleluya! Wa maisha ya daima. Amenena mwenyewe, Haleluya! Utaishi ukitazama. Tazama! Ishi sasa! Kumtazama Ywsu. Amenena mwenyewe, Haleluya! Utaishi ukitazama. Ni ujumbe wa wema , Haleluya! Nawe shika, rafiki yangu, Ni habari ya raha, Haleluya! Mwenye kuisema ni Mungu. Tazama … Uzima wa daima, Haleluya! Kwake Yesu utauona. Ukitazam tu, Haleluya! Wokovu pekee wa Bwana. Tazama …

74. Bwana Uliyewaita Watakatifu

Bwana uliye waita, Watakatifu wako, Wawe mitume, wachunga, Walishe kundi lako; Wanyonge na wenye hofu Wakawa mashujaa, Na wapole wa kunena Wasiwe kunyamaa. Hata leo wawataka Watakatifu wako, Nawe wauliza tena Ni nani aliyeko Atakaye ni mtume Afundishe vijana? Ni tayari Bwana wangu Ni tume mimi Bwana. Nitume na mimi, Bwana, Kama ulivyotumwa, Habari za msamaha, Na dhambi kutubiwa, Niwahubiri wakosa, Na waliopotea, Wokovu u wake Bwana, Aliyewafilia. Astahiliye hapana Kutanka habari, Lakini Wawe waweza Kutufanya tayari Neno lako tulijue, Tupe na Roho wako, Hayatakuwa ya bure, Haya maneno yako.

75. Mikononi mwa Mitume

Mikononi mwa mitume Kazi ilifanywa, si nguvu yao Walipewa msaada, ndiye  Roho. Wakapata kuona upya tena. /: Nenda, (kazini tu) nenda, (siache) kuyasema.:/ Sisi ni badala yao. Mitume wa zamani Tupe vipawa vya kazi, /:tuifanye (tuifanye) Kazi yako (kazi yako):/ Ututume, ututume, ututume Tuombe kupata Roho Tuende kazini. Si nguvu yetu Kwa kufanya kazi hii Njema mno. Tutakwenda haraka Kuifanya. Nenda, nenda … Vuvia Roho Mtakata Ndani mioyoni utuhuishe Tupe moto wa Roho, Tusimame Tuwe tayari kwenda Kutumika. Nenda, nenda …

76. Mwana Kondoo Ayalipa

Mwana Kondoo ayalipa Madeni ya dunia. Ayachukua makosa Ya wakosaji wote. Aenda na kuugua, Anakubali kuchinjwa, Furaha aziacha. Wanamhukumu wampiga, Wanamtukana wamtesa, Asema: nakubali. Mwana Kondoo ni Mwokozi Ni Mponya wa mioyo; Aliyetumwa na Mungu Awakomboe watu. Mwanangu, nenda okoa Watoto niliotupa. Sababu ya makosa. Dhambi zao ni nyingi mno; Watolee ukombozi Damu na mwili wako. “Tayari mimi, Babangu, Nitwishe nichukue, Maneno uyasemayo Nitafuata yote” Pendo hili kubwa sana, Lamsjika Baba wa mbingu Amtoe mwana wake. Pendo hili lina nguvu, Linamlaza kaburini Aletaye uzima. Sitasahau pendo hili Bwanangu siku zote, Nitakushika daima, Kama unishikavyo. Mwanga war oho ni wewe; Roho inapozimia Niwie moyo wangu. Na tuagane, Bwanangu, Na halafu mbingini.

77. Mwana Kondoo wa Mungu Waiondoa Dhambi

Mwana Kondoo wa Mungu Waiondoa dhambi; Tuhurumie Mwana Kondoo wa Mungu Waiondoa dhambi; Tuhurumie. Mwana Kondoo wa Mungu waiondoa dhambi; Ututulize. Amen.

78. Mwokozi Wangu Umekosa Nini?

Mwokozi wangu umekosa nini? Wahukumiwa kama mwuaji. Umeshtakiwa makosa Mangapi uliyotenda? Wapigwa sana, Miiba taji lako, Umetemewa mae, Watukanwa, Wanyweshwa nyongo Tena siki kali, Sababu gani Unateswa hivi? Makosa yangu yanakuumiza; Mateso haya yako yanipasa, Mimi mkosaji. Ajabu kwabwa Sana tendo lako; Mchungaji unateswa kwa ajili ya kondoo, Bwana Unawalipia watumwa wako. Tulipokuwa mateka Wa mwovu, Nawe ukaja ukatukomboa. Tulistahili kufa kwa milele, Ukatufia. Mwokozi wangu nifanyeje mimi, Niitangaze pote sifa yako? Nakufuata nikutumikie Maisha yote.

79. Nakusalimu Kichwa

Nakusalimu kichwa Kilichojaa damu, Kilichovikwa taji La miiba mikubwa, Kilichopata enzi Kwa Mungu mbinguni, Kitukanwacho sasa Matusi makali. Naona uso wako watemewa mate, Watemewa mate, Heshima yako yote Imeondolewa. Mwanga wa macho yako Wazimika sasa. Aliyekuharibu hivi, Ndiye nani? Mateso yako Bwana, Yanipasa mimi. Wewe waadhibishwa Kwa ajili yangu. Hukumu unapata iliyonipasa. Bwananangu nakuomba, Unihurumie! Na mimi nasimama msalabani pako; Niwe karibu kwako utoapo roho; Ukiugua sana kwa teso la kufa, Nitakushika Bwana Kwa moyo wa pendo. Bwana nayashukuru Masumbuko yako, Sababu ya kuteswa Na kufa kuchungu. Wewe umenishika, Nami nakushika, Mwisho nitakufia Uliyenifia. Moyo unaposhikwa Na woga wa kufa, Usiniache Bwana Katika vita hii. Siku ya kufa kwangu Unisaidie, Kufa kwako kuchungu Kutaniokoa. Niwie kama ngao Nitakapo kufa, Nione uso wako Katika uchungu. Ndipo nikutazame Nikukumbatie! Anaye kufa hivi Afa kwa amani.

80. Liko Neno Moja Nipendalo

Liko Neno moja nilipendalo Ni chakula cha moyo; Neno hili linanituliza Nikipatwa na shida: Kumtazama Bwana wetu pale, Atoapo jasho kama damu, Akubalipo mzigo, Baba aliomtwika. Siku zote namkumbuka yeye, Alivyosulubishwa, Akivumilia taabu kimya Kama mwana wa kondoo. Name akanikumbuka mimi, Alisema: yamemalizika! Huko aliniteka, Name niwe mtu wake. Bwana wangu u mwenye huruma, Mimi ni mkosaji tu; Nilipokuwapo oenye giza Wewe ukatokea, Ukamtafuta kondoo wako, Kabla mimi sijakusikia. Watoa ukombozi Unipao uhuru. Ndimi huru lako, Bwana Yesu, Wewe ndiwe Bwanangu. Jina lako, boea liung’aze Moyo wangu vizuri. Amani yako nikae nayo, Siku zangu zote mpaka kufa. Ndivyo ninavyoomba, Bwana unikubali.

81. Ulimwengu Tazama

Ulimwengu tazama, Yesu Mwokozi wako asulubiwavyo, Mwenye heshima yote anayavumilia Mateso tena matusi. Karibia tazama maungo yake Yote yatokavyo damu. Na moyo wake mwema Kwa shida na uchungu Unaungua vigumu. Nani akupigaye, Aliyekufanyia Mambo kama haya? Wewe huna makosa Kama wengine wote, Hujui kosa lolote. Makosa yangu mimi Yaliyo kama mchanga Hayahesabiki, Ndiyo yakutiayo mateso Na uchungu Uliyo ya vumilia Mimi nimestahili Kulipa haya yote, Na kufungwa sana. Mapigo na mateso Uliyopata wewe Yalitoka kwangu mimi. Umenitwika mzigo Ulio mzito sana Kuliko jiwe kuu. Wachukua maovu, Tupate kuokoka Tukae nawe daima!

82. Mwana Kondoo wa Mungu Unachinjwa

Mwana kondoo wa Mungu Unachinjwa msalabanai Wavumilia sana Ujapodharauliwa, Waichukua dhambbi, Tupate kuokoka. Utuhurumie Yesu. Mwana Kondoo wa Mungu Unachinjwa msalabani Wavumilia sana Ujapodharauliwa Waichukua dhambi, Tupate kuokoa. Utuhurumie Yesu. Mwana Kondoo wa Mungu Unachinjwa msalabani Wavumilia sana Ujapodharauliwa Waichukua dhambi, Tupate kuokoa. Tutulize mioyo, Yesu.

83. Yesu, Kuteswa Kwako

Yesu, kuteswa kwako nitakufikiri Nipe kwa shauri hili Roho na mbaraka. Moyo wangu uone hali yako Yesu Jinsi ulivyoteswa Kwa ajili yetu. Moyo wangu uone Taabu yako kubwa, Maumivu, mapigo, Na kuwambwa mtin, Taji lako la miiba Tena misumari, Iliyokuumiza, Hata kufa kwako. Nikitazama yote Yaliyokutesa, Nifikiri sababu Na maana yake. Sababu ndio mimi Na makosa yangu; Umepata mateso, Nipate huruma. Yesu unifundishe Nijui kwa moyo; Nisikuzidishie Shida na uchungu. Nisiweze kupenda Yaliyokutesa: Nataka kuyaacha Na kukufuata.

84. Nimshangilie Bwana Wangu

Nimshangilie Bwana wangu Na kumwimbia Mkombozi Katukomboa msalabani, Nisifu pendo lake kuu Haya mwimbieni Yesu, Amekubali mateso, Katukomboa msalaabani, Tusifu pendo lake kuu! Tumsifu yeye Mponya wetu Katika ulimwemgu huu, Katupatanisha na baba, Tulio wakosaji tu. Haya mwimbieni … Katuletea mwanga wake, Tulikaa katika giza, Wokovu ukaonekana, Kamshinda mwovu, Ni shujaa! Haya mwimbieni … Na tumtukuze Bwana wetu, Tumtumikie kwa bidii, Na atawale apendavyo, Na sisi sote tutamtii! Haya mwimbieni …

85. Uliyesulubishwa

Uliyesulubishwa, Mtakatifu bwanangu, Uwe ngao shidani, Uniombee mimi. Uliyesulibushwa, Mtakatifu Bwanangu! Wongofu sina hata Niondolee makosa. Mwovu akinishtaki, Nasumbuka rohoni. Wongofu sina hata, Niondolee makosa. Wewe tu nipokee, Nakukimbilia wewe, Hata nifanye bidii, Nikatoe machozi. Wewe tu nipokee, Nakukimbilia wee. Uwe ngao shidani, Niombee na mimi! Hapa nikiumizwa, Saa ya mwisho ikija: Uwe ngao shidani, Niombee na mimi!

86. Roho Yangu Tua Hapa

Roho yangu tua hapa Mlimani pa Golgota, Angalia tendo hili, Afanyalo mfalme mkuu. Amevutwa na upendo Kuacha enzi yake. Yesu alivyotupenda, Twaona msalabani, Maumivu hata manza Ya makosa yampata. Anakaa mahali petu, Sikia ateswavyo! Kufa kwako kunivute Nife pamoja nawe Mwili na mapenzi yangu Yakazikwe nawe Bwana. Niwe na kutengemana, Mwenye pendo la kweli!

87. Ee, Watoto Njooni

Ee, watoto njooni, Njooni Golgota, Mtazameni Yesu aumizwavyo! Mtazameni huko Mkamtazame, Sogeeni kwake, Ametupenda. Sogeeni kwake, Mkamtazame, Mioyo iyeyuke, Mwangukieni! Mioyo imlilie Anayeteswa; Mzigo wetu mkubwa Aukubali. Mizigo wa makosa Ya ulimwengu. Mpeni nanyi nyote Mioyo yenu! Apata mshahara, Nikufa kwake: Wewe una raha, Kwake ni kufa. Ataona enzi Ya utukufu. Tuimbe haleluya Na kumshukuru

88. Nataka Kusimama

Nataka kusimama Chini ya msalaba, Kama kivuli cha mwamba Wakati wa mchana, Kama ni maji nyikani, Kambi safarini, Na hapa nitapumzika, Kwani jua kali. Mahali pema sana Chini ya msalaba, Kwani hapo waoneka Upendo wa Yesu. Yakobo alivyoona Ndotoni zamani, Mti Yesu aliowambwa, Ni ngazi kwa Mungu. Juu ya msalaba huo Yesu alikufa. Alikufa tuokoke, Tuliopotea. Ninastaajabu kabisa Ni mambo mawili: Kwake Yesu ni upendo, Kwangu mimi kosa! Wataka kuonana Na Yesu Mbinguni, Yakupasa kukaa kwanza Chini ya mti huo. Ni kwake siku chache tu Mateso na shaka. Halafu pasipo mwisho Furaha kwa Bwana!

89. Kumbuka Getsemane

Kumbuka Getsemane, Asongapo Shetani, Mwokozi ukamwone Ateswavyo shambani; Nao uchungu wewe, Aombapo kumbuka! Kumbuka barazani Ashtakiwapo Yesu; Mtazame Bwana huko, Walipomhukumia; Upate soni wewe, Mti wa Yesu Kumbuka! Kumbuka na Golgota Alipokufa Bwana. Upaji wa tambiko Ameutoa yeye. Kasema: imekweisha Mti wa Yesu Kumbuka! Kumbuka bustanini Walipomzika Yesu, Kukiwa bado giza. Mfu amekwenda wapi? Amefufufuka yeye; Ufufuo Kumbuka!

90. Mtini Mponya Alipowambwa

Wimbo: Unter dern Kreuze wo Jesus Starb. N.K. 71, C.H. 259 Mtini Mponya alipowambwa, ndipo nimwombapo upozi akaniokoa mpenzi. Mwana wa Mungu. Mwana wa Mungu Mwokozi wangu. Mtini Mponya alipowambwa, Mwana wa Mungu Chini ya mti wenye uchungu, ndipo nimwombapo usafi, mara kwa damu kaniosha Mwana wa Mungu. Mwana wa Mungu. Akaniondolea manza, ameingia ndani mwangu, kwani mtini amenifia. Mwana wa Mungu. Mwana wa Mungu Ziwa la damu ya kaisi, linatosha makosa yote, laniendesha wokovuni. Mwana wa Mungu. Mwana wa Mungu Hicho kijito chenye mali! U tayari kuzama humo? Humo utaona uzima! Mwana wa Mungu. Mwana wa Mungu

91. Ni Damu Idondokayo

Wimbo:  The is a fountain. R.I. 175, S.S.&S. 129, N.K. 229 Ni damu idondokayo mwilini mwa Yesu, wakosaji wakioga, husafishwaji kweli. Bwana wangu Mungu wangu, u uzima wangu, umekutana na kufa kwa ajili yangu! Ilimpatia wokovu mwizi kule mtini; name nisiyemtafuta, inanisafisha. Bwana wangu Shaushi aliyemlinda Yesu akiteswa, naye akamshuhudia: ni mwana wa Mungu! Bwana wangu Nipe ulimi mpya Yesu wa kukuimbia, Babayo tutamtukuza Jina lake pekee. Bwana wangu

92. Ukiwa na Vichache

N.K. 73,. H.C. 96  Mtunga sauti. S. Salvatori Ukiwa na vichache umtolee Bwana, kwani akiba yako ataiongeza. Vipaji vyako haba yeye hakatai, kidogo kwako wewe, kwake kitazidi! Vile vile na moyo umtolee Bwana! Ndivyo vipaji vyema vinavyompendeza. Kwani sisi wenyewe alitukomboa, akiuawa yeye kwa kuwambwa mtini. Ukiwa na ubaya umwambie Bwana! Ukishindana nao, atakutakasa. Damu aliyotoa, ndiyo itoshayo, kuosha wakosaji, hata wewe vivyo. Vitu vya mali nyingi umtolee Bwana! Alitoka mbinguni kusumbuka hapa. Alikufa mwenyewe kwa ajili yako, nawe hutoi chako kwa ajili yake? Wakristo na tutoe shukrani kwa Mungu. Hiyo ndiyo shukrani ya wokovu wetu. Injili yake Kristo, ienee pote! Kwa ushuhuda wetu watu waokoke.

93. Njoo Msalabani

Sauti na wimbo: Kifransa N.K. 74, T.B. 165, R.I. 150 Wimbo asili: E.L. Budly, 1854 – 1932 Njoo msalabani ukilemewa, wewe msafiri! Kwenye msalaba utapumzika, ndiyo raha. Wamwona Mwana Kondoo wa Mungu, akichukua mshahara mkuu wa makosa yako, akufia Yeye asiye mkosaji hata, ahukumiwa, Waona jinsi akupendavyo ewe mdhambi?

94. Unipe Nguvu Bwana

Unipe nguvu, Bwana nikumbuke mateso yako yaliyokupata, kutukomboa tulioanguka katika dhambi. Umemtii Baba, mpaka kufa kwako mahali petu ulisulubishwa, makosa yetu yalikuwa mengi, umetufia. Wokovu wangu ulinitafuta; nakuangukia Mwokozi wangu, nakushukuru nikiitazama huruma yako.

95. Bwana Yesu Alikufa

Bwana Yesu alikufa kwa sababu yetu sisi, alipata duniani maumivu mengi sana. Bustanini akiomba akafadhaika kabisa. Jasho lake kama damu nchini ikadondoka. Wayuda wakamwendea, wakamshika, wakamfunga, na rafiki zake wote wakimbia, wakamwacha. Na wale wakampeleka barazani kumhukumu. Wamhukumu yule mfalme, atakayewahukumu. Wakamfyonza, wakampiga, wakampeleka Golgota, pale wakamwamba mtini, kwa misumari kumkaza. Kukawa na giza huko, nchi ikatetemeka. Watu walioko wote, wakaona woga mwingi. Na saa tisa ikifika, Yesu apaza sauti kuu, kwamba: Yamemalizika; mara akakata roho. Askari wakamwendea, wakamwona amekufa. Nao wakamchoma mkuki; ukapenya moyo wake. Damu yake ikatoka, yakatoka maji tena. Maji, damu iwezayo kuosha uchafu wote. Na watu wema wamshusha, wamfunga katika sanda, wakamweka kaburini, na penye mlango jiwe kuu. Siku ya tatu atoka Yesu Kristo kuzimuni, alivyotangaza kwanza, yu mzima hata milele!

96. Wakristo Twabeba Nini?

K: Wakristo twabeba nini? W: Msalaba wake Yesu: Twaenda twashutumiwa. K: Wakristo twavaa nini? W: Twavaa vazi la Yesu: Twaenda twashutumiwa. K. Wakristo twaenda wapi? W: Twaenda njia ya Yesu, ni njia yenye mateso. K: Mwokozi twamwona pale, W: Ateswapo Goligota; Kwa uchungu anapita K: Wakristo tuvumilie W: Njia hii yenye shida, Mwisho wake tutashinda. K: Tushinde kw anguvu gani? W: Yesu ni ushindi wetu. Katoa ahadi kwetu. K: Mwokozi wetu kashinda W: Mauti nalo kaburi. Yu hai hata milele.

97. Mwana Kondoo wa Mungu Uichukuaye Dhambi

Mwana Kondoo wa Mungu uichukuaye dhambi yote, mwana Kondoo wa Mungu, uturehemu wakosaji, Mwana Kondoo wa Mungu. Mwana Kondoo wa Mungu uichukuaye dhambi yote, Mwana Kondoo wa Mungu, uturehemu wakosaji, Mwanakondoo wa Mungu. Mwana Kondoo wa Mungu, uichukuaye dhambi yote, Mwana Kondoo wa Mungu Utupe amani yako, Mwanakondoo wa Mungu. AMEN

98. Mungu Ameona Tulivyo

K: Mungu ameona W: Tulivyo huku chini, K: Neno hilo jema W: Litokalo mbinguni Ya kwamba Yesu kaja na kutuongoza, tufike uzimani. K: Hujui njia W: Uende upande gani K: Nuru yake Bwana W: Huangaza njiani. Ya kwamba Yesu K: Kweli, unajua, W: Mtu wa duniani. K: Atakuongoza W: Upate kuamini. Ya kwamba yesu. K: Njooni tufungue W: Milango ya moyoni K: Neno lake Bwana W: Likaingie ndani. Ya kwamba Yesu

99. Yesu Alitufia

Asili ya Wimbo: Haijulikani Yesu alitufia, tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; tumshangilie Yesu Mwokozi. Sisi watu wabaya, tumshukuru Tumshukuru Wakamvua mavazi, tumshukuru! Tumshukuru Walimchezea Bwana, tumshukuru! Tumshukuru Aliteswa Golgotha, tumshukuru! Tumshukuru Kasema imekwisha, tumshukuru! Tumshukuru Hakushindwa na kifo, tumshukuru! Tumshukuru. Katoka kaburini, tumshukuru! Tumshukuru Kafufuka kwa wafu, tumshukuru, tumshukuru Ndiye Mwokozi wetu, tumshukuru! Tumshukuru Ataishi milele, tumshukuru! Tumshukuru

100. Mungu Tusaidie

Asili ya Wimbo: Haijulikani Mungu tusaidie, sisi tunaangamia. Nchi imeharibiwa na mwovu wake shetani. Kweli kweli ndiye Yesu aliyewambwa mtini penye mlima wa Golgotha aokoe wenye dhambi. Kaonyesha huruma, wayuda wamsumbua. Wakampiga makofi, Pilato aliamua. Kweli kweli ndiye Yesu Yesu mwenye upendo alikubali kuuawa, damu ilimwagika ili sisi tuokoke. Kweli kweli ndiye Yesu. Pale msalabani, Bwana Yesu aliteswa mzigo wa dhambi zetu ulimwangukia yeye. Kweli kweli ndiye Yesu Sote na tukumbuke, kifo cha Mwokozi wetu. Alisema ya kwamba jililieni wenyewe. Kweli kweli ndiye Yesu Habari zilisemwa. Mahali hapa hayupo, ona alipokuwa, jiwe limeondolewa. Kweli kweli ndiye Yesu Ni ajabu kabisa wingu kuja kumpokea, habari ilisema Yesu atarudi tena. Kweli kweli ndiye Yesu

101. Moyo Wangu Amka Hima

Moyo wangu amka hima, jua limetokea. Ondoka usingizini, mpokee Mponya wako, atokaye kaburini, kashinda nguvu za kifo, watu wafurahishwe. Fufuka pamoja naye, uyaache mabaya! Maliza mwenendo wako ukimgojea Yesu, aliyekwenda mbinguni. Kwa hiyo nawe ufanye yampendezayo yeye. Ukiwa na wasiwasi Yesu anauweza; Ukipatwa na huzuni, yeye furaha yako. Umtwike Bwana mizigo. Usisumbuke: yu hapa, kwani amefufuka. Usimwogope Shetani, kifo hata kuzimu. Shida za kufa nyepesi mwokozi Yesu ni mzima. Shujaa wetu haondoki, awagombea wanyonge wanaomtumaini.

102. Haleluya Tumwimbie

Haleluya! Tumwimbie tumsifu sana Bwana wetu, tumshangilie kwa shangwe. Akafungwa na adui alipokufa msalabani, lakini sasa yu hai. Habari njema hii: Mesiya anakaa mzima kweli. Haleluya! Tumsifu! Tumsifu! Mungu wetu. Haleluya! Tumwimbie, tumsifu sana Bwana wetu, tumshangilie kwa shangwe. Watu wana shida sana, taabu nyingi na huzuni mpaka watakapokufa. Furaha yetu hii; Bwana ametoka kaburini. Haleluya! Tumsifu! Tumsifu Mungu wetu! Haleluya! Tumwimbie, tumsifu sana Bwana wetu, tumshangilie kwa shangwe. Atatufufua sisi, tutafika rahani kwake, tuishi pamoja naye. Tumwamini yeye Mwokozi wetu mkuu, mwenye nguvu. Haleluya! Tumsifu! Tumsifu Mungu wetu!

103. Moyo Yafurahie, yafanywayo

Moyo yafurahie, yafanywayo leo; mwanga umetokea gizani mwa kufa, Mwokozi kalazwa, tutakapozikwa, roho ikiisha kurudi mbinguni. Alipozikwa yeye adui acheka. Lakini akashindwa; Kristo afufuka. Atokea shujaa bendera mkononi, kwani ameteka mateka ya mwovu. Ni jambo kubwa hili lenye furaha kuu. Sitaogopa sasa uchungu wa kufa, na yote mengine yatakayotokea mali nipewayo na Yesu Mwokozi. Namshika siku zote Mwokozi wangu mkuu, yeye ni kichwa chetu sisi tu viungo. Dunia, makosa Shetani, na kufa yeye kawashinda, name namfuata. Afika furahani name nitafika, sitaona huzuni na shida zozote. Mkubwa wangu Yesu atanikingia vinavyonidhuru, yeye ngao yangu. Nitakapoingia mbinguni, naona andiko la furaha linasomwa hivi: ashindaye kule aingia hapa, anayejidhili atakuzwa hapa!

104. Yesu Amefufuka

Yesu amefufuka, sitakuogopa kufa, amefufuka, naye atanifufua mimi. Atanipa mwili mpya; ni tumaini langu. Yesu amefufuka, anapatawala pote, name nitatawla pamoja naye milele. Atimiza agano; ni tumaini langu. Yesu amefufuka, yanipasa kumngojea. Mwenye kumtegemea Bwana wetu, ataona rehema yake Mungu; Ni tumaini langu. Yesu amefufuka, naweza kumtumikia, nashindana na tama, moyo wangu uwe safi. Atanisaidia; ni tumaini langu. Yesu amefufuka, siwezi kutengwa tena na Yesu Bwana wangu. Kwa mateso au furaha. Vyote havinishindi; ni tumaini langu. Yesu amefufuka, ni mlango wa kuingia furahani mbinguni. Nitatulizwa nikifa, nikiweza kusema; u tumaini langu!

105. Leo Shangwe Zitolewe

Leo shangwe zitolewe shujaa atoka kufani. Mtumishi wa Bwana huyu aone kushinda kwake shangwe shangwe! Shangwe, shangwe zitolewe! Imbeni haleluya! Mwana Kondoo amekuwa leo samba mwenye nguvu. Jiwe kubwa halimwezi, kaburi lamfungukia. Shangwe shangwe Bwana Yesu umeshinda, utupe uliyoteka; utengemano wa Mungu uliopata vitani! Shangwe, shangwe Yesu tunakutukuza, twataka utugombee. Tuweze kushinda nawe, kwa kuwa sisi tu wako. Shangwe shangwe

106. Ameshafufuka Kristo kaburini

Ameshafufuka Kristo kaburini, kwa hiyo twafurahi, tunapata upozi. Uturehemu! Asingefufuka sote tungepotea, alivyotoka kufani, sisi tunamtumaini uturehemu! Tumsifu Bwana! Tumsifu Bwana! Kwa hiyo twafurahiwa. Yesu ni mtulizaji! Uturehemu!

107. Kumekucha, ni Mzima

Kumekucha, ni mzima Yesu aliyefufuka. Kaburi lake wazi, kufa hakumshiki Yesu. Sina woga na kifo, Yesu amefufuka. Kumekucha, ni mzima Yesu aliyefufuka! Tunaitwa nduguze, sababu anatupenda. Tusiachane naye, yeye aliyeshinda. Kumekucha, ni mzima Yesu aliyefufuka. Kamba zitufungazo zimekwisha funguliwa mwili wangu uoze, sina woga na kufa!

108. Tumfurahie Daima

Tumfurahie daima, Yesu aliyefufuka Haleluya! Haleluya! Giza haliwezi kukaa, jua limelifukuza. Haleluya!Haleluya! Haleluya!Haleluya!Haleluya Nao moyo wa Maria, unashangilia sana, Haleluya! Haleluya! Nayo mioyo yetu sisi, inapiga shangwe nyingi! Haleluya!. Jeraha zake za kufa, zatupatia uzima, Haleluya!Haleluya! Na sasa anatawala katika enzi ya Baba. Haleluya! Mwokozi hakuogopa, kuvuka maji ya kufa, Haleluya! Haleluya! Atupa nasi moyo mkuu, Tuongoze tufike juu! Haleluya!

109. Tumsifu Mungu Enzini

  Tumsifu Mungu enzini na Mwana wake wa pekee, aliyefanya wokovu: Haleluya! Haleluya! Haleluya! Siku ya tatu mapema, jiwe halijaondolewa, akafufuka mshindaji. Haleluya! Haleluya! Ametoka kuzimuni, makosa hata shida zote, zimetoweka kabisa. Haleluya! Haleluya! Haleluya! Umemwumbua Shetani, ukamvua mapambo yake, ukafungua kifungo. Haleluya! Haleluya!

110. Haleluya, Haleluya

Haleluya, Haleluya, sauti na mioyo juu, tumwimbie Mungu nyimbo tumsifu na furaha, aliyemwaga damuye kwa ulimwengu wote, mefufuka kifoni sas Yesu Mwokozi. Minyororo yake kifo imekatika pia, na katika wafu wote yee mzaliwa wa kwanza Yesu ameshinda sasa, nasi twashinda naye. Ametupatia nasi uzima wa milele. Kristo afufuka kwanza nao wengi baadaye. Atakapokuja tena, watatokea naye, mavuno yatakuwako mwisho wa ulimwengu, watafika furahani wote watakatifu. Mwokozi amefufuka, nasi tutafufuka, tunyeshee kama mvua neema yako ee Bwana. Tutafute yaliyo juu, siyo ya ulimwengu, na uzima tutapewa naye Kristo kwa Mungu. Tumsifu, tumsifu Mungu wetu, apaswa. Tumsifuni na Mwokozi, aliyeshinda vita. Tumsifu naye Roho, kisima cha mapenzi. Tumsifu Mungu wetu, ni Utatu wa enzi.

111. Siku ya Furaha (Yesu Kristo Afufuka)

Siku ya furaha, siku ya uzima, Yesu Kristo afufuka! Watu kifungoni, wamefunguliwa, furahini, furahini Wakristo! Siku ya furaha, siku ya uzima, Yesu Krisyo afufuka! Kufa kumeshindwa, uzima tayari! Furahini, furahini Wakristo! Siku ya furaha, siku ya uzima, Yesu Kristo afufuka! Nguvu twapokea, kumfuata sasa. Furahini, furahini Wakristo!

112. Leo Siku ya Furaha

Leo siku ya furaha, kila mtu ashangilie, Kristo afufuka, ateka adui wote! Haleluya! Nyoka wa kale na kifo, kuzimu hata ubaya vimeshindwa na mshindaji Yesu Kristo Mfalme wetu! Haleluya! Mateka yote ya kifo yamekamatwa na Yesu, na ufu umenyang’anywa naye aliyefufuka! Haleluya! Adui hawatushiki tunakwenda uzimani, tunapokunywa naye kinywaji kipya milele! Haleluya! Jua na mwezi na nchi, viumbe vyote vya Mungu vinafurahiwa leo; Mfalme wa uongo ashindwa! Haleluya! Kwa hivi tushangilie, tumwimbie Yesu Kristo, yeye ametuokoa, afufuka kaburini! Haleluya!

113. Bwana Yesu Kafufuka

K: Bwana Yesu kafufuka, ametoka kaburini. W: Haleluya, Haleluya, ametoka kaburini K: Na mashaka yalizuka, hapakuwa tumaini, W: Haleluya, Haleluya, ametoka kaburini K: Wanawake walifika asubuhi kaburini.  W: Haleluya, Haleluya, ametoka kaburini K: Tayarini waliweka manukato mkononi.  W: Haleluya, Haleluya, ametoka kaburini K: Walitaka kuupaka mwili mle kaburini.  W: Haleluya, Haleluya, ametoka kaburini K: Nao hao walifika; kumbe jiwe li kandoni.  W: Haleluya, Haleluya, ametoka kaburini K: kwa ukweli malaika kasimama kaburini.  W: Haleluya, Haleluya, ametoka kaburini K: Wakasema kafufuka; enyi nyote kumbukeni.  W: Haleluya, Haleluya, ametoka kaburini K: Wanawake wakumbuka; wakatoka kaburini.  W:Haleluya, Haleluya, ametoka kaburini K: Kweli Yesu kafufuka, ametupa tumaini.  W: Haleluya, Haleluya, ametoka kaburini K: Atazidi kw aneema kuokoa waamini.  W: Haleluya, Haleluya, ametoka kaburini

114. Amefufuka Katika Wafu

1. K: Amefufuka katika wafu, akiwa na utukufu.  Kristo pekee, ndiye mwenye nguvu.  W: Yeye limbuko la waliolala,  tena ni mwisho wa nguvu ya mauti kwetu. 2. K: Hii ni habari iliyo kweli, iletayo udhahiri.  Yapasa wote, tuache mashaka.  W: Yesu pekee ndiwe ustahiliye kushika mamlaka yote. 3. K: Kristo u Bwana mwenye uweza.  Shetani umemshinda, kazi yote umeimaliza.  W: Uhimidiwe, ewe Bwana pekee, utupokee tunapokuja kwako, Bwana. 4. K: tuutangaze ushindi wake, mataifa waje kwake,  wafahamu utukufu wake.  W: Asante, Bwana, kwa ushindi wako kwa watu wako. Shetani hana nguvu tena.

115. Yesu, Yesu Amefufuka

K: Yesu, Yesu  W: amefufuka.  K: Yesu, Yesu  W: amefufuka ameshinda dhambi na mauti, amefufuka. 1. K: Akina baba tumwendee  W: Amefufuka.  K: Akina mama tumwendee  W: amefufuka.  K:Na sisi sote tumwendee  W: amefufuka.  K: Yesu, Yesu 2. K: Ujifunue na kwetu,  W: Mwokozi wetu  K: Utupe wokovu wako  W: Mwokozi wetu,  K: Twakuamini, ee Bwana  W: Mwokozi wetu  K: Yesu, Yesu,  W: amefufuka Ushindaji wako huokoa Yesu Mwkozi. 3. K: Twakungojea kwa shangwe,  W: Yesu Mfalme  K: Fahari yako tuone,  W: Yesu Mfalme  K: Na tukusifu daima,  W: Yesu Mfalme  K: Yesu, Yesu,  W: Umefufuka.  K: Yesu, Yesu,  W: Umefufuka sisi sote utatufufua siku ya mwisho.

116. Amefufuka Kweli

1. K: Amefufuka  W: Kweli Yesu amefufuka kutoka wafu.  K: Kaburi tupi.  W: Staajabuni nyote juu ya mwujiza huu.  K: Bwana Yesu  W: Hayupo kaburini  K: Yu hai  W: Yu mzima daima.  K: yeye ndiye  W: Pekee kashinda kifo. 2. K: Sisi Wakristo  W: Tufurahi kwa shangwe kubwa siku ya leo,  K: Sababu Kristo  W: Amemshinda Mfalme mkuu wa dunia hii. K: Yeye ndiye  W: Shetani mbaya sana.  K: Anapenda  W: Kuwadanganya Wakristo  K: Waiache  W: Njia yenye uzima. 3. K: Ssa wenzangu  W: Twende sote tumtumikie Mfalme wetu.  K: Tuwatafute  W: Watu wengi wanaopotea maovuni.  K: Tuwaletee  W: Kwake Yesu Mwokozi  K: Washiriki  W: Nasi furaha hii  K: Haleluya,  W: Kristo amefufuka. 4. K: Mungu apenda  W: Watu wote wafike kwake kwa kumwamini  K: wakamwambie  W: Kwa shukrani, kwani amewashindia vita,  K: Tumuombe  W: Yesu asaidie,  K: Tuushinde...

117. Yesu Amefufuka (Haya Shangilia)

1. K: Yesu  W:Amefufuka, ametoka kaburini  K: Haya,  W: Shangilia,   K: Haya,  W: Shangilia, ametoka kaburini. 2. K: Shetani  W: AMeshindwa.  K: Shetani  W: Ameshindwa hana lake duniani  K: Haya,  W: shangilia,  K: Haya  W: Shangilia, ametoka kaburini. 3. K: Yesu  W: Kawatokea,  K: Yesu  W: Kawatokea wanafunzi wake wote  K: Haya,  W: Shangilia  K: Haya  W: Shangilia ametoka kaburini. 4. K: Amani  W: Iwe kwenu,  K: Amani  W: Iwe kwenu Mpokee Roho wangu.  K:Haya,  W: Shangilia, K: Haya  W: Shangilia, ametoka kaburini. 5. K: Bwana  W: Yesu kapaa, sasa yu juu mbinguni  K: Haya,  W: Shangilia, sasa yu juu mbinguni. 6. K: Sasa  W: Kristo huketi,  K: Sasa  W: Kristo huketi kuumeni mwake Baba  K: Haya,  W: Shangilia,  K: Haya  W: Shangilia, sasa yu juu mbinguni. 7. K: Hivyo  W: Anatawala,  K: H...

118. Mle Kaburini Yesu Mwokozi

1. Mle kaburini Yesu Mwokozi! Alilazwa chini. Bwana wangu! Bwana amefufuka, kifo kimeshindwa kabisa! Gizani mle alitoka chini, sasa atawala huko mbinguni! Yu hai! Bwana Yesu yu hai. 2. Aungoja huo, Yesu Mwokozi Mchana ujao, Bwana wangu! Bwana! Amefufuka,…………………….. 3. Walinda kaburi, Yesu Mwokozi! Bure ni muhuri, Bwana wangu! Bwana! Amefufuka,……………… 4. Kifo kimeshindwa, Yesu Mwokozi! Pingu zimevunjwa, Bwana wangu! Bwana! Amefufuka,……….

119. Bwana Amefufuka, Haleluya

1. Bwana amefufuka, haleluya. Tuimbe na amlaika, haleluya. Sifa zetu na shangwe, haleluya. Na zao zisitengwe. Haleluya. 2. Ukombozi timamu, haleluya. Umetimu kwa damu, haleluya. Mshindi asifiwe, haleluya. Yu hai kwa milele, haleluya. 3. Jiwe, lindo, muhuri, haleluya vi wapi? Na kaburi? Haleluya. Kifo hakimuwezi, haleluya. Ametoka kuzimu, haleluya. 4. Yu hai mtukufu, haleluya. Cha kifo hatuofu! Haleluya. Alitufia sisi, haleluya. Tuwe huru na sisi, haleluya. 5. Kichwa chatangulia, haleluya. Tupate, nasi pia! Haleluya. Kw akuwa tuna fungu, haleluya. Mti, kaburi mbingu, haleluya. 6. Ndiwe mwokozi wetu, haleluya. Sifa ni yako Yesu, haleluya. Utukuzwe pekee, haleluya. Ni wewe ufufuo, haleluya.

120. Ameingia Mbinguni

1. Ameingia mbinguni. Haleluya Kristo mwenye utukufu. Haleluya. 2. Akaa kitini kwa Mungu Haleluya! Mkuu wa dunia na mbingu. Haleluya! 3. Sasa limetimilika. Haleluya! Agano lote la kale. Haleluya! 4. Mwana Daudi, Mfalme mkuu. Haleluya! Sasa ni Bwana wa wote haleluya! 5. Sababu hii tumsifuni. Haleluya! Yesu Mwokozi wetu mkuu! Haleluya!

121. Mwokozi Wetu Amepaa

1. Mwokozi wetu amepaa mbinguni!  Neno hili linatufariji sasa katika woga wote.  Kikiwa kichwa mbinguni,  hata viungo vyafika alikokwenda yeye. 2. Mwokozi wetu amepaa mbinguni,  mwenye nguvu mbinguni nitapokewa nitengemane kweli.  Sababu hii ninataka kufika pale alipo Mwokozi wangu Yesu. 3. Mwokozi wetu amepaa mbinguni!  Nakuomba Mwanangu!  Nisaidie nikutegemee weee.  Nikufuate daima mwisho nifike kwako juu nikiacha dunia.

122. Shujaa Mkubwa

1. Shujaa mkubwa, Bwana wetu, leo umejikalisha kitini kwa babako,. Ufalme wote ni wako, umeshinda maadui, hawana nguvu tena, umepewa enzi kubwa, kufa pia uzima, vyote unavitawala. 2. Malaika wote wa mbingu wanakusifu wanakusifu kwa nyimbo wanakutumikia. Ulipotoka mbinguni ukaja kutuokoa, na umerudi leo. Sasa, wako utukufu, nasi tunakushukuru, tunasifu jina lako. 3. Twataka kutafuta tu ufalme wako wa mbingu. Utupe nguvu zako, tushike mwenendo mwema, tusiwe wenye kiburi ila wanyenyekevu. Tuepuke kila kosa, tufuate njia yako ya kuingia mbinguni. 4. Yesu mwana wa Daudi uliyetupatanisha na Bwana Mungu wetu. Ulipokwenda mbinguni umetutengenezea makao ya milele. Tuongoze, tusichoke, tusafiri siku zote, kwani watungoja kwako.

124. Mbinguni Nani?

1. K: Mbinguni nani? W: Mbinguni amepaa. Ni Yesu kwa Baba. K: Akawa wapi? W: Akawa kwa watu, wamtia maumivu, akayalipa madeni makubwa, na Mungu ampaza; Aha! Mtawala! 2. K: Wenzangu nani? W: Wenzangu waenda, waenda mbinguni. K: Na tuwe kwa Yesu, aliyetulinda. Hapa duniani. Sasa tunamsifu Mwokozi wetu Mkuu aha, yuko juu! KUIMBA KWA KIFUKUZANO 1. Mbinguni nani, Mbinguni amepaa ni Yesu kwa Baba, akawa wapi, akawa wapi, akawa kwa watu, wamtia maumivu, akayalipa madeni makubwa, na Mungu ampaza, aha, mtawala 2. Wenzangu nani, wenzangu waenda, waenda mbinguni, na tuwe wapi, na tuwe wapi, na tuwe kwa Yesu aliyetulinda hapa duniani, sasa tunamsifu, Mwokozi wetu Mkuu aha, yuko juu.

125. Tazameni, Anapaa

1. Tazameni, anapaa, mwenye kushinda vita; gari lake ni mawingu, ndipo anapopita; Malaika wa Mbingu wakimwimbia Bwana; Amekaribishwa sasa, kwa kufurahi sana. 2. Ni nani anayepaa, wote wakimsifu? Ndiye Bwana mwenye enzi, ndiye Mungu wa safu, aliyeteseka kwanza mle katika mti, kwa kifo chake mwenyewe, akashinda Mauti. 3. Akaaga watu wake, na akawabariki  akapaa Mawinguni na wakimwangalia, chini hutenda ya Mungu, yote yakatimia; Kazi yake imekwisha, kwake amerejea. 4. Ni Kuhani wetu sasa,yumo na Damu yake, katika patakatifu twapatanishwa kwake; Amefanya ukombozi kuondoa dhambi zetu;  Mungu amekubali ndiye sadaka yetu. 5. Mwili ameuinua huo wa ki-Adamu ndani yake sisi sote pia tuna sehemu, Mingu na mtu mmoja, yuko huko enzini twaamini Bwana, kwamba tutakwenda Mbinguni.