71. Wajibu Mwema Watoka Kwako



K:   Wajibu mwema watoka kwako,

Bwana mwenye utukufu.

Neno jema ndilo jina lako.

W:  /:Yesu ni mwanzo

wa kazi shamabni,

tena ni Bwana,

wa nguvu kwa utume wetu:/


K:   Watendakazi mwako shambani,

Uwape matumaini.

Nazo nguvu wakiwa kazini.

W:   /: Watende yote kwa uaminifu,

Wawe makini,

Huduma isiharibike. :/


K:  Wapate heri

kuyasikia uliyo yaagizia.

Waje nao kutuhubiria.

W:  /: Tena kazini

Wakaelexee Neno

Kwa wazi, na kweli

Ya uzima wako. :/


K:   Wajihadhari wawe

Na hamu,

Kushika na kufahamu.

Jina lako lika warehemu.

W:   Ni wachungaji,

Waju hilo tu

Si watawala.

Bwana, ujifunue kwao.:/


K:   Unawatuma

Katika kundi,

Kwa bidii na juhudi.

Nasi kwao

Tuwe mashahidi.

W:   /: Ushangiliwe

Kwa neema yako,

Na kundi lako

Lijue lina viongozi:/

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu