58. Jina Moja ni Kubwa sana



Jina moja ni kubwa sasa;

Ni jina lako Bwanangu!

Nasifu jina hili lako,

Yesu Kristo u Mwokozi.

Li tamu kwangu jina hili,

Jina lingine silijui.


Naliandika jina hili

Rohoni mwangu kabisa.

Silisahau siku zote,

Halifutiki moyoni.

Li tamu kwangu jina hili,

Jina lingene sitafuti.


Jina hili ni jua langu

Lawaka ndani ya roho.

Lanipa na utengemano,

Lafuta makosa yote.

Li tamu kwangu jina hili,

Jina linguine sifahamu.


Jina hili ni boma langu,

Upanga wangu vitani,

Ni ngao yangu na silaha,

Lamshinda hata Shetani.

Li tamu kwangu jina hili,

Jina linguine silitaki.


Jina hili lanipa nguvu,

Niweza kwenda kwa haki.

Ujuzi wote umo humo

Katika jina la Yesu.

Li tamu kwangu jina hili,

Jina linguine sitamani.


Ee Yesu, jina lako ndilo

Furaha yangu nikifa.

Ni cheti cha kuingilia

Mbinguni kwa Bwana

Mungu

Ndipo nitalisifu sana,

Jina linguine silijui.

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu