4. Fungua Milango Yote



Fungua milango yote

Yuaja Bwana wa mbingu,

Mfalme wa wafalme wote,

Mwokozi wa ulimwengu.

Atuletea uzima;

Kwahiyo tumuimbieni;

Tumsifuni Mungu,

Aliye tuumba.


Ni mwenye haki na shujaa

Uple mwingi amevaa;

Rehema ni taji yake;

Huruma ni fimbo yake;

Atuondolea shida.

Kwahiyo tumuimbieni;

Tumsifuni Mungu,

Mwokozi watu mkuu.


Miji na nchi

Huchipuzwa,

Afikako Mfamle huyu;

Nayo mioyo huchekeshwa,

Anayo ingia Yesu.

Ndio jua la furaha

Linalo tufurahisha.

Tumsifuni Mungu

Mtunza mioyo yetu.


Fungua milango yote!

Tengenezeni mioyo!

Makuti yawe upole,

Furaha, pendo, amni.

Mwokozi ata wajia,

Aleta raha, uzima.

Tumsifuni Mungu,

Ni mwenye rehema.


Njoo, mwokozi wangu Yesu,

Nakufungulia moyo.

Uingie na rehema,

Nione upole wako.

Uniongoze kwa roho,

Nifike kwako Mbinguni.

Jina lako Bwana

Lisifiwe pote.

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu