24. Ulimwenguni Pote
Ulimwenguni pote
Asifiwe Mungu mkuu
Amemtuma Mwokozi,
Wakosaji wapone.
Zamani wazee wale
Wameona hamu kuu,
Waondoshwe makosa
Na kumpata Mwokozi.
Abrahamu, Yakobo
Na watu wa sayani
Walimngojea sana,
Sasa umetujia.
Karibu mponya wangu
Niondolee woga.
Ujitengenezee
Njia moyoni mwangu.
Safisha nyumba yako
Umfukuze Shetani,
Yule nyoka wa kale.
Nikutumikie wee!
Comments
Post a Comment