60. Ufalme wa Mungu
Ufalme wa Mungu
uenee popote!
Nguvu yako iokoe
wakaao gizani.
Uondoe woga wote,
ukawape watu uzima,
ufalme wa Mungu.
Ushinde upesi!
Uharibu ufalme
wa shetani duniani,
ndiye mfalme wa giza.
Nawe utamshinda yeye,
Kwani una nguvu ya Mungu
Ushinde upesi!
U Shujaa wa Mungu!
Kwa rehema ya Bwana
urudishe watu wako’
wapendane kwa moyo,
wawe raia wako pote.
Ndipo utatukuzwa sana!
U shujaa wa Mungu!
Duniani popote
jina lako livume
nguvu zako zi sifiwe
na makabila yote,
uliowatengemaza,
mpaka utakapo tawala
duniani popote!
Shikeni amri hii:
Tangazeni popote
kwa makabila yoyote
neno lenye furaha,
wapate kuokolewa.
Yesu alivyotuagiza.
Shikeni amri hii!
Sifuni rehema
Ya kuokoa watu!
Tukimtumikia Bwana.
azibariki kazi
zote za mikono yetu;
Amani kuu iwe kwetu.
Sifuni rehema!
Comments
Post a Comment