78. Mwokozi Wangu Umekosa Nini?



Mwokozi wangu umekosa nini?

Wahukumiwa kama mwuaji.

Umeshtakiwa makosa

Mangapi uliyotenda?


Wapigwa sana,

Miiba taji lako,

Umetemewa mae,

Watukanwa,

Wanyweshwa nyongo

Tena siki kali,


Sababu gani

Unateswa hivi?

Makosa yangu yanakuumiza;

Mateso haya yako yanipasa,

Mimi mkosaji.


Ajabu kwabwa

Sana tendo lako;

Mchungaji unateswa kwa ajili ya kondoo,

Bwana

Unawalipia watumwa wako.


Tulipokuwa mateka

Wa mwovu,

Nawe ukaja ukatukomboa.

Tulistahili kufa kwa milele,

Ukatufia.


Mwokozi wangu nifanyeje mimi,

Niitangaze pote sifa yako?

Nakufuata nikutumikie

Maisha yote.

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu