37. Sote Tufurahi



K:  Sote tufurahi,

W: Habari ni njema

K:  Njoni nyote wahi,

W: Tupate uzima.

Sasa yametimia

Yaliyotabiriwa.

Mwokozi kazaliwa.


K:  Kule Bethlehemu

W: Yesu kazaliwa

K:  Mama Mariamu

W: Alivyoambiwa.

Sasa yametimia….


K:  Kumbe, huyo Mwana

W: kazaliwa horini

K:  Huyo Yesu Mwana

W: akawa shidani.

Sasa yametimia…


K: Mwana atiiye

W: ni Bwana shujaa,

K:  Kwake tuwe wana,

W: ni Mponya dunia.

Sasa yametimia….


K:  Jeshi la mbinguni

W: katoa Injili.

K:  Watu walishoni,

W:  kaona ni kweli.

Sasa yametimia…


K:  Mungu yupo nasi

W: katika dunia.

K:  Pendo kwa waasi,

W: katoa kwa nia.

Sasa yametimia…..


K:  Raha na tushike,

W: tunaye Masihi

K:  Haya twende kwake

W: sauti zasihi.

Sasa yametimia…..


K: Wote wenye Mwana

W: wanao uzima.

K: Yeye ndiye Bwana,

W: atoa karama.

Sasa yametimia…..


K:  Nyota yatunuka

W: shinani mwa Yese

K:  Bwana atukuka,

W: akatutakase.

Sasa yametimia...


K: Sasa, ndugu nyote,

W: tangaza neema.

K:  Waje kwake wote

W:  tupate rehema.

Sasa yametimia….


Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu