102. Haleluya Tumwimbie
Haleluya! Tumwimbie tumsifu
sana Bwana wetu, tumshangilie
kwa shangwe. Akafungwa na adui
alipokufa msalabani,
lakini sasa yu hai.
Habari njema hii: Mesiya anakaa
mzima kweli. Haleluya!
Tumsifu! Tumsifu! Mungu wetu.
Haleluya! Tumwimbie,
tumsifu sana Bwana wetu,
tumshangilie kwa shangwe.
Watu wana shida sana,
taabu nyingi na huzuni mpaka
watakapokufa. Furaha yetu hii;
Bwana ametoka kaburini.
Haleluya! Tumsifu!
Tumsifu Mungu wetu!
Haleluya! Tumwimbie,
tumsifu sana Bwana wetu,
tumshangilie kwa shangwe.
Atatufufua sisi,
tutafika rahani kwake,
tuishi pamoja naye.
Tumwamini yeye Mwokozi wetu mkuu,
mwenye nguvu. Haleluya!
Tumsifu! Tumsifu Mungu wetu!
Comments
Post a Comment