16. Tunakuamkia Yesu
Tunakuamkia Yesu
Tunakupa pongezi.
Umezaliwa kikiwa,
Malaika wakuabudu,
Uwe nasi!
Mwana na Mungu wa pekee,
Yeye ni mgeni wetu,
Anajiunga na sisi
Mfalme wa kale na kale!
Uwe nasi!
Ashikaye ulimwengu
Ashikwa na Maria!
Ni mtoto mdogo na mchanga!
Tena ni Bwana wa mbingu!
Uwe nasi
Nuruu ya milele aja
Kuleta mwanga wake
Aondoa giza lote;
Tuwe watoto wa mwanga.
Uwe nasi!
Kwetu akawa maskini
Kwa kutuhurunia,
Tupate mali ya mbingu,
Tuwe watoto wa Mungu.
Uwe nasi!
Amefanya haya yote
Kwa kuwa atupenda.
Kwa hiyo furahini tu
Na tumshukuru daima!
Uwe nasi!
Comments
Post a Comment