95. Bwana Yesu Alikufa
Bwana Yesu alikufa kwa sababu
yetu sisi, alipata duniani
maumivu mengi sana.
Bustanini akiomba akafadhaika
kabisa. Jasho lake kama damu
nchini ikadondoka.
Wayuda wakamwendea, wakamshika,
wakamfunga, na rafiki zake wote
wakimbia, wakamwacha.
Na wale wakampeleka barazani
kumhukumu. Wamhukumu yule mfalme,
atakayewahukumu.
Wakamfyonza, wakampiga,
wakampeleka Golgota,
pale wakamwamba mtini,
kwa misumari kumkaza.
Kukawa na giza huko,
nchi ikatetemeka.
Watu walioko wote,
wakaona woga mwingi.
Na saa tisa ikifika,
Yesu apaza sauti kuu, kwamba:
Yamemalizika; mara akakata roho.
Askari wakamwendea,
wakamwona amekufa.
Nao wakamchoma mkuki;
ukapenya moyo wake.
Damu yake ikatoka,
yakatoka maji tena.
Maji, damu iwezayo
kuosha uchafu wote.
Na watu wema wamshusha,
wamfunga katika sanda,
wakamweka kaburini,
na penye mlango jiwe kuu.
Siku ya tatu atoka
Yesu Kristo kuzimuni,
alivyotangaza kwanza,
yu mzima hata milele!
Comments
Post a Comment