10. Bwana Anakuja
Bwana anakuja
Twendeni kumlaki
Bwana wangu wa majeshi.
Iwasheni mioyo
Tukampokee
Huyo mwenye utukufu.
Karibu Bwana, njoo
Karibu Bwana, njoo
Shinda pamoja nasi.
Wewe ndiwe mfalme,
Mfale wa mbinguni
Utulishe wenye njaa.
Wewe ndiwe mwanga,
Sisi tu vipofu
Tufanye tuone tena
Wewe ndiwe njia,
Tuta kufuata
Turudi kwa baba yetu.
Wewe ndiwe kweli,
Utuangazie
Tusije tukapotea.
Hosanna, Hosana,
Huyo mbarikiwa
Anakuja kwetu sisi.
Aja kutulisha na kutugawia
Matunda ya ukombozi.
Comments
Post a Comment