50. Twapenda Ukaapo



Twapenda ukaapo

Bwana wetu enzini,

Furaha zako wewe

Zinazipita zote.


Palipo pa kuomba

Wajapo watu wako

Na wewe Bwana upo,

Uwakubali wote.


Twapenda neno lako,

Habari za wokovu,

Za nguvu za kushinda,

Za shangwe za mbinguni.


Twapenda nyimbo zako,

Tunaziimba hapa,

Mpaka tutaziimba

Pamoja na malaika.


Utujalie Yesu,

Tuzidi kukupenda,

Tuone uso wako

Utakavyotakata.

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu