74. Bwana Uliyewaita Watakatifu
Bwana uliye waita,
Watakatifu wako,
Wawe mitume, wachunga,
Walishe kundi lako;
Wanyonge na wenye hofu
Wakawa mashujaa,
Na wapole wa kunena
Wasiwe kunyamaa.
Hata leo wawataka
Watakatifu wako,
Nawe wauliza tena
Ni nani aliyeko
Atakaye ni mtume
Afundishe vijana?
Ni tayari Bwana wangu
Ni tume mimi Bwana.
Nitume na mimi, Bwana,
Kama ulivyotumwa,
Habari za msamaha,
Na dhambi kutubiwa,
Niwahubiri wakosa,
Na waliopotea,
Wokovu u wake Bwana,
Aliyewafilia.
Astahiliye hapana
Kutanka habari,
Lakini Wawe waweza
Kutufanya tayari
Neno lako tulijue,
Tupe na Roho wako,
Hayatakuwa ya bure,
Haya maneno yako.
Comments
Post a Comment