55. Mmoja Ndiye
Mmoja ndiye
Tumpendaye
Aliyetoa mwili wake
Akikubali mateso.
Twakupa mioyo yetu
Mwokozi uliyetufia,
Twapenda kuwa wako tu.
Bwana tukubali!
Ututengeneze sisi wako.
Nuru yako itung’aze
Tusipotee gizani,
Sisi hatukukuita,
Ila umetuita wewe,
Huruma yako ni kubwa.
Nguvu zetu hazitoshi,
Kukufanyia kazi njema
Usipotutia nguvu.
Shida yetu sisi
Ndio ulegevu, uondoe;
Nia zetu zigeuzwe
Tufanye kazi kwa bidii.
Yesu, wewe umesema:
‘’Watenda kazi ni wachache
Kweny mavuno ya Bwana’’
Twaomba: Tutume nasi,
Tualike wageni wengi,
Nyumba ya Bwana ijae.
Heri watu wale
Uliochagua kuja kwako
Kwenye raha na furaha,
Milele hata milele.
Uwahurumie watu
Walio mbali na wokovu
Wanaoshikwa nagiza.
Hawajasikia bado
Utume mwema wa wakovu
Tunaopewa na Mungu.
Jua la uzima
Liche hata kwao.
Njoo Mwokozi!
Tangulia! Twafuata,
Ukifungua milango.
Tunataka kutangaza
Habari ya upendo wako,
Ya moyo wako wa kweli
Tutawaonyesha watu
Msalaba wako siku zote,
Mpaka washindwe mioyoni,
Kwani neno lako
Lina nguvu kubwa ya
Kushinda.
Mzigo wako ni mwepesi.
Mlango wa mbinguni ni wazi.
Comments
Post a Comment