101. Moyo Wangu Amka Hima
Moyo wangu amka hima,
jua limetokea. Ondoka usingizini,
mpokee Mponya wako,
atokaye kaburini,
kashinda nguvu za kifo,
watu wafurahishwe.
Fufuka pamoja naye,
uyaache mabaya! Maliza mwenendo
wako ukimgojea Yesu, aliyekwenda
mbinguni.
Kwa hiyo nawe ufanye yampendezayo yeye.
Ukiwa na wasiwasi Yesu anauweza;
Ukipatwa na huzuni, yeye furaha yako.
Umtwike Bwana mizigo.
Usisumbuke: yu hapa, kwani amefufuka.
Usimwogope Shetani,
kifo hata kuzimu.
Shida za kufa nyepesi mwokozi
Yesu ni mzima. Shujaa wetu haondoki,
awagombea wanyonge wanaomtumaini.
Comments
Post a Comment