66. Mfalme ni Yesu Pekee



Mfalme ni Yesu pekee,

Wote wanamwangukia,

Watawalishwa na Mungu,

Ndimi zote ziungame

Yesu ni Mfalme wa pekee,

Atukuzwe popote.


Maflme mkubwa,

Watu wako

Wakutii, wanakusifu.

Yesu apita wafalme,

Yeye ndiye mkubwa sana,

Apenda kuwakomboa,

Kwani ndiye Mwokozi.


Enyi watu mpeni mioyo,

Mnaohuzunika njooni,

Wakiwa semeni naye,

Kwani vyote aviweza

Awagawia uzima

Wanaomngoja yeye.


Kama wataka uzima,

Nenda kwake, acha soni,

Yeye anakungoja.

Amejitoa mwenyewe,

Wewe upate kurithi

Mbingu ni yako sasa.


Nimsifuje Yesu Kristo

Mimi vumbi, mimi jivu?

Nasema: nitamtangaza

Kristo Yesu ndiye Bwana!

Na tumpende,

Tumheshimu

Sifa zote zampasa.

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu