33. Niende na Wachungaji
Niende na wachungaji
Nimtazame mponya wangu,
Kazaliwa duniani
Kwa kunipenda mimi.
Nimwimbie na malaika,
Niusifu utukufu.
Anautengemaza
Kila moyo unipende.
Nikawaze na Maria
Jambo hili la ajabu:
Acha mwili mzuri,
Achukua wa kimtu.
Nimpelekee vipaji
Na watambuzi wa nyota,
Na nimpe maji yangu,
Hata uzima nimpe.
Nakupenda, u Mwokozi,
Nikumbuke siku hii.
Uje mwangu moyoni,
Uufanye kikao.
Comments
Post a Comment