67. Nyesha Mvua



Nyesha mvua, nyesha mvua,

Wewe Roho wa Baba,

Nchi kavu ikanyweshwe,

Insifu Mungu wetu!


Vuma sana, vuma sana

Roho mwenye uzima,

Tulio na usingizi

Utuamshe kwa mkono!


Toa mwanga, toa mwanga,

Roho kwani unang’aa

Wewe ushinde usiku

Tusikae na giza.


Sikiliza, sikiliza,

Wewe Mflme wa mbingu!

Tuma Roho wako kwetu,

Kote kuwe na upya!

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu