108. Tumfurahie Daima



Tumfurahie daima, Yesu

aliyefufuka Haleluya! Haleluya!

Giza haliwezi kukaa, jua limelifukuza.

Haleluya!Haleluya!

Haleluya!Haleluya!Haleluya


Nao moyo wa Maria, unashangilia

sana, Haleluya! Haleluya!

Nayo mioyo yetu sisi,

inapiga shangwe nyingi! Haleluya!.


Jeraha zake za kufa, zatupatia uzima,

Haleluya!Haleluya! Na sasa anatawala

katika enzi ya Baba. Haleluya!


Mwokozi hakuogopa, kuvuka maji ya kufa,

Haleluya! Haleluya! Atupa nasi

moyo mkuu, Tuongoze tufike juu!

Haleluya!

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu