12. Njooni, Tumheshimu Yesu
Njooni, tumheshimu Yesu,
Tumtolee sifa zetu,
Tumwimbie kwa furaha,
Sisi watu wa Yesu.
Baba amemtuma Mwana
Atuletee uzima,
Utakao pewa watu
Wenye shida na kufa.
Moyo wake watupenda
Kwa upendo amekuja,
Aokoe wenye dhambi
Wasishindwe na mwovu.
Nuru imetutokea,
Yesu akiponda kichwa
Cha adui wetu mkali
Anayetudanganya.
Tuta barikiwa kweli,
Tukishika neon hili,
Tukimsifu Bwana Yesu
Kwa vyinywa na mioyo.
Mwana mzuri Bwana Yesu,
Twakuomba tupeleke
Pale wakuimbiapo
Malaika nyimbo nzuri
Comments
Post a Comment