61. Sifuni Nyote Huruma
Sifuni nyote huruma ya Mungu,
Kwa nyimbo nzuri,
Umati wa Yesu!
Atualika furahini:
/:Msifuni Bwana kwa neema yake:/
Yeye ni Mfalme
Anaye tawala;
Viumbe vyote
Vinamtumikia,
Hata malaika,
Wamwabudu,
/:wanambwimbia kwa sauti nzuri:/
Enyi amataifa,
Hofu iacheni!
Njooni kwa Yesu,
Mchunga kondoo mwema.
Sikilizeni Neno lake:
/:Atukomboa kwa kufa kwake:/
Awapa watu chakula chochote,
Atushibisha kama baba mzuri,
Aleta jua hata mvua,
/:Atubariki kwa wema wake:/
Sifuni nyote huruma ya Mungu,
Kwa nyimbo nzuri,
Umati wa Yesu!
Sasa huzuni twaishinda:
/:Msifuni Bwana neema yake!:/
Comments
Post a Comment