65. Yesu ni Mponya
Yesu ni Mponya,
Aleta furaha!
Mwanzo na mwisho
Wa vyote ndiye.
Mwana Adamu
Na Mungu wa kweli
Ametujia atubariki.
Mbingu, dunia,
Toeni habari:
Yesu ni Mponya,
Aleta furaha!
Yesu ni Mponya
Aleta wokovu!
Sikilizeni habari njema!
Sisi tulipomwacha
Mungu wetu
Akaturudisha tena kwake.
Ametufanya watoto
Wa Mungu. Yesu ni Mponya
Aleta wokovu.
Yesu ni Mponya,
Aleta uzima
Kamba za kufa zimekatika.
Mwana wa Mungu
Kumshinda Shetani,
Awakomboe watumwa wake,
Amewapata, kawapa uhuru.
Yesu ni Mponya,
Aleta uzima
Yesu ni Mponya,
Mchungaji wa kweli,
Amaye lisha vizuri kondoo.
Wote walio mbali awaita,
Awarudishe kundini mwake.
Awakomboa kondoo kuani:
Yesu ni Mponya
Mchungaji wa kweli.
Yesu ni Mponya
Na mfalme wa enzi!
Mbingu zimsifu na watu wamtii
Anageuza mioyo ya watu,
Hata na sisi tumpe yetu,
Kwani apenda kutupa uzima.
Yesu ni Mponya
Na Mfalme wa enzi!
Yesu ni Mponya
Na mwenye upendo!
Anatupenda
Kwa moyo wote.
Yeye mwenyewe.
Upendo wa kweli,
Aliyekufa kwa kutupenda.
Nasi tumpendaye kwa nguvu ya roho!
Yesu ni mponya na mwenye upendo.
Comments
Post a Comment