62. Uamke Kwetu Tena Roho



Uamke kwetu tena Roho

Wa mashahidi wale kwanza,

Waliolesha siku zote,

Waliomshinda Yule adui,

Wakihubiri Neno la Yesu

Kwa watu wa ulimwengu wote.


Uwashe moto wa Upendo,

Uendelee pote kuwaka.

Peleka watu mavunnoni,

Wanao fanya kazi kwa bidii.

Bwana mwenye mavuno,

Tazama:

Watenda kazi yako ni haba.


Mwanao ametuagiza

Kuomba hivi kwa Jina lake,

Na sisi wanafunzi wake,

Twashika Neno Lake kwa bidii.

Twaomba hivi kwa moyo wote.

Ee Bwana usikie, ufanye!


Utume watu wengi sana,

Walitangaze Neno kwa nguvu.

Tusaidie, tuokoe;

Ufalme wa Shetani uishe.

Usimamishe, Bwana wa mbinguni,

Ufalme wako

Ulimwenguni!


Utume mwema na uende

Mahali popote huku nchini.

Wadiini zote waingie,

Kundini mwako mwa wateule.

Amsha nao Wana wa  ahadi

Na wa Imani zote wakutii.

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu