104. Yesu Amefufuka
Yesu amefufuka, sitakuogopa kufa,
amefufuka, naye atanifufua mimi.
Atanipa mwili mpya; ni tumaini langu.
Yesu amefufuka, anapatawala pote,
name nitatawla pamoja naye milele.
Atimiza agano; ni tumaini langu.
Yesu amefufuka, yanipasa kumngojea.
Mwenye kumtegemea Bwana wetu,
ataona rehema yake Mungu;
Ni tumaini langu.
Yesu amefufuka, naweza kumtumikia,
nashindana na tama, moyo wangu uwe safi.
Atanisaidia; ni tumaini langu.
Yesu amefufuka, siwezi kutengwa
tena na Yesu Bwana wangu.
Kwa mateso au furaha. Vyote
havinishindi; ni tumaini langu.
Yesu amefufuka, ni mlango wa
kuingia furahani mbinguni.
Nitatulizwa nikifa, nikiweza
kusema; u tumaini langu!
Comments
Post a Comment