125. Tazameni, Anapaa



1. Tazameni, anapaa, mwenye kushinda vita; gari lake ni mawingu, ndipo anapopita;


Malaika wa Mbingu wakimwimbia Bwana; Amekaribishwa sasa, kwa kufurahi sana.


2. Ni nani anayepaa, wote wakimsifu? Ndiye Bwana mwenye enzi, ndiye Mungu wa safu, aliyeteseka kwanza mle katika mti, kwa kifo chake mwenyewe, akashinda Mauti.


3. Akaaga watu wake, na akawabariki  akapaa Mawinguni na wakimwangalia, chini hutenda ya Mungu, yote yakatimia; Kazi yake imekwisha, kwake amerejea.


4. Ni Kuhani wetu sasa,yumo na Damu yake, katika patakatifu twapatanishwa kwake; Amefanya ukombozi kuondoa dhambi zetu;  Mungu amekubali ndiye sadaka yetu.


5. Mwili ameuinua huo wa ki-Adamu ndani yake sisi sote pia tuna sehemu, Mingu na mtu mmoja, yuko huko enzini twaamini Bwana, kwamba tutakwenda Mbinguni.


Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu