2. Hosiana, Mesiya
Hosiana, Mesiya
Aingia mjini kwake
Fagieni popote,
Zipambeni njia zote;
Tandikeni mauwa,
Aingie na shwangwe.
Hosiana,Mwokozi
Njoo, twakungojea Bwana.
Tumepamba nioyo,
Twakukaribisha kwetu.
Tunakufungulia, milango ya mioyo
Hosina, ee shujaa!
Utusaidie sisi,
Tuwe wako kwa kweli
Tukutumikie vema.
Kwani hutakubali
Watu wasio kutii.
Hosiana, Mfalme mkuu!
Uingie kwetu hima!
Uliebarikiwa,
Uingie mlango wetu.
Hosiana, karibu!
Bwana, njoo! Haleluya!
Comments
Post a Comment