122. Shujaa Mkubwa



1. Shujaa mkubwa, Bwana wetu, leo umejikalisha kitini kwa babako,. Ufalme wote ni wako, umeshinda maadui, hawana nguvu tena, umepewa enzi kubwa, kufa pia uzima, vyote unavitawala.


2. Malaika wote wa mbingu wanakusifu wanakusifu kwa nyimbo wanakutumikia. Ulipotoka mbinguni ukaja kutuokoa, na umerudi leo. Sasa, wako utukufu, nasi tunakushukuru, tunasifu jina lako.


3. Twataka kutafuta tu ufalme wako wa mbingu. Utupe nguvu zako, tushike mwenendo mwema, tusiwe wenye kiburi ila wanyenyekevu. Tuepuke kila kosa, tufuate njia yako ya kuingia mbinguni.


4. Yesu mwana wa Daudi uliyetupatanisha na Bwana Mungu wetu. Ulipokwenda mbinguni umetutengenezea makao ya milele. Tuongoze, tusichoke, tusafiri siku zote, kwani watungoja kwako.


Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu