15. Tawi Limechipuka
Tawi limechipuka
Shinani mwa Yese,
Kama tulivyopashwa
Habari na wazee.
Likatoa ua
Wakati wa usiku
Lilipochanua.
Isaya alitaja ua hilo zuri.
Ni Yesu, mponya wetu,
Maria alimzaa
Usiku mtulivu.
Uwezo wake Mungu
Umefanya hivi.
Na ua hili dogo
Lanukia vyema;
Lang’aa kama jua
Giza lakufukuzwa.
Ni Mwana wa Mungu,
Hata mwana Adamu;
Mwokozi wa watu.
Siku ya kufa kwetu
Yesu tuongoze,
Tuiache dunia,
Twende furahani
Mbinguni kwa Mungu
Pale tuta kusifu
Pasipo kukoma.
Comments
Post a Comment