103. Moyo Yafurahie, yafanywayo



Moyo yafurahie, yafanywayo leo;

mwanga umetokea gizani mwa kufa,

Mwokozi kalazwa, tutakapozikwa,

roho ikiisha kurudi mbinguni.


Alipozikwa yeye adui acheka.

Lakini akashindwa; Kristo afufuka.

Atokea shujaa bendera mkononi,

kwani ameteka mateka ya mwovu.


Ni jambo kubwa hili lenye furaha kuu.

Sitaogopa sasa uchungu wa kufa,

na yote mengine yatakayotokea

mali nipewayo na Yesu Mwokozi.


Namshika siku zote Mwokozi wangu mkuu,

yeye ni kichwa chetu sisi tu viungo.

Dunia, makosa Shetani,

na kufa yeye kawashinda, name namfuata.


Afika furahani name nitafika,

sitaona huzuni na shida zozote.

Mkubwa wangu Yesu atanikingia

vinavyonidhuru, yeye ngao yangu.


Nitakapoingia mbinguni,

naona andiko la furaha linasomwa hivi:

ashindaye kule aingia hapa,

anayejidhili atakuzwa hapa!

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu