20. Njooni Wachungaji Bethlehemu!
Njooni wachungaji
Bethlehemu!
Njooni kumtazama mototo
Mzuri
Mwana wa Mungu
Amezaliwa.
Baba amtuma awakomboe.
Msiogope!
Anatujia atufurahishe
Njooni tumtukuze!
Zienezwe popote sasa:
Yesu mponya kaja
Yesu mponya kaja.
Usiku mtakatifu!
Siku ya furaha
Imetuangaza kimungu
Tumeupewa ukombozi
Kristo amefika
Kristo amefika.
Twnde Bethlehemu
Tukaone
Tulivyoambiwa na malaika.
Tuyaonayo tutatangaza
Na kutukuza kwa nyimbo
Nzuri
Haleluya!
Kweli malaika
Wametangaza
Furaha kubwa kwa
Wachungaji.
Comments
Post a Comment