80. Liko Neno Moja Nipendalo
Liko Neno moja nilipendalo
Ni chakula cha moyo;
Neno hili linanituliza
Nikipatwa na shida:
Kumtazama Bwana wetu pale,
Atoapo jasho kama damu,
Akubalipo mzigo,
Baba aliomtwika.
Siku zote namkumbuka yeye,
Alivyosulubishwa,
Akivumilia taabu kimya
Kama mwana wa kondoo.
Name akanikumbuka mimi,
Alisema: yamemalizika!
Huko aliniteka,
Name niwe mtu wake.
Bwana wangu u mwenye huruma,
Mimi ni mkosaji tu;
Nilipokuwapo oenye giza
Wewe ukatokea,
Ukamtafuta kondoo wako,
Kabla mimi sijakusikia.
Watoa ukombozi
Unipao uhuru.
Ndimi huru lako,
Bwana Yesu,
Wewe ndiwe Bwanangu.
Jina lako, boea liung’aze
Moyo wangu vizuri.
Amani yako nikae nayo,
Siku zangu zote mpaka kufa.
Ndivyo ninavyoomba,
Bwana unikubali.
Comments
Post a Comment