81. Ulimwengu Tazama
Ulimwengu tazama,
Yesu Mwokozi wako asulubiwavyo,
Mwenye heshima yote anayavumilia
Mateso tena matusi.
Karibia tazama maungo yake
Yote yatokavyo damu.
Na moyo wake mwema
Kwa shida na uchungu
Unaungua vigumu.
Nani akupigaye,
Aliyekufanyia
Mambo kama haya?
Wewe huna makosa
Kama wengine wote,
Hujui kosa lolote.
Makosa yangu mimi
Yaliyo kama mchanga
Hayahesabiki,
Ndiyo yakutiayo mateso
Na uchungu
Uliyo ya vumilia
Mimi nimestahili
Kulipa haya yote,
Na kufungwa sana.
Mapigo na mateso
Uliyopata wewe
Yalitoka kwangu mimi.
Umenitwika mzigo
Ulio mzito sana
Kuliko jiwe kuu.
Wachukua maovu,
Tupate kuokoka
Tukae nawe daima!
Comments
Post a Comment