59. Kazi ni Yako Bwanangu
Kazi ni yako Bwanangu tunayoifanya;
Hakuna ayeweza
Kuvunja kazi hii.
Ni kama punje ya mbegu
ikiwa ndani ya mchanga,
inakufa kwa kuoza;
na hapo yabadilika,
inaota, yakua na kuzaa.
Yesu umeteswa kwanza,
Halafu umepaa.
Nao wakufuatao
Wanateswa vivyo.
Twaomba tusaidie
nasi tushike njia hii,
kwa kufa kwako na sisi
tunatoka kaburini.
Tuongoze, tufike mbinguni.
Bwana wewe umekufa
kwa ajili yetu
Ukaweka ufufuo
ulipofufuka.
Twaomba: Tuma motume,
wajulishe jina lako
mpaka mwisho wa dunia.
Utakubali na sisi
kwa kazi hii,tutume,
twakutii!
Comments
Post a Comment