112. Leo Siku ya Furaha
Leo siku ya furaha,
kila mtu ashangilie,
Kristo afufuka, ateka
adui wote! Haleluya!
Nyoka wa kale na kifo,
kuzimu hata ubaya vimeshindwa
na mshindaji Yesu Kristo
Mfalme wetu! Haleluya!
Mateka yote ya kifo
yamekamatwa na Yesu,
na ufu umenyang’anywa
naye aliyefufuka! Haleluya!
Adui hawatushiki tunakwenda
uzimani, tunapokunywa naye
kinywaji kipya milele! Haleluya!
Jua na mwezi na nchi, viumbe
vyote vya Mungu vinafurahiwa
leo; Mfalme wa uongo ashindwa!
Haleluya!
Kwa hivi tushangilie,
tumwimbie Yesu Kristo,
yeye ametuokoa, afufuka
kaburini! Haleluya!
Comments
Post a Comment