46. Twendeni Tumshukuru
Twendeni tumshukuru
Na kumwimbia Mungu,
Aliyetupa roho
Na nguvu mpaka leo.
Twaenda na kukua
Miaka yetu yote,
Hivyo mwaka kwa mwaka
Twafikia uzee.
Twaona shida nyingi,
Uchungu na mateso
Na vita na misiba
Katika ulimwengu.
Kuhangaika kwetu
Siku zote ni bure
Asipotushikiza
Yeye atulindaye,
Na kama mama mwema
Anavyomlinda mtoto
Katika shida zote,
Asipotee njia.
Hivyo na Mungu wetu
Hulinda watu wake,
Huwakingia shida,
Huzuni na misiba.
Huruma zako ni mpya
Kila panapokucha,
Hizo zinakomesha
Uchungu wa mioyo.
Utabariki sote
Katika njia zetu,
Wakubwa kwa wadogo
Wakalishe mwangani.
U baba wa wakiwa,
U mshauri wa wajinga,
U mponya wa wagonjwa,
U msaada wa maskini.
Na mwisho twakuomba;
Utupe roho yako,
Atufundishe hapa,
Atuongoza kwako.
Wewe mwenye uzima
Utupe haya yote
Sisi wakristo wako!
Kwani twakungojea!
Comments
Post a Comment