34. Wakristo Furahini



Wakristo furahini,

Furahini sana!

Mwaipigiwa leo

Mbiu yenu njema!

Malaika wanaimba

Huko juu mbinguni,

/:wanaimba vizuri

Sauti ya kushangaa!:/


Hivi wanavyoimba:

Furahini nyote!

Acheni kuogopa,

Tazama nyote

Kwani amezaliwa

Mwokozi wa pekee:

/: ni Bwana Yesu Kristo,

Mwana Mungu wetu!:/


Shangilieni nyote

Na kusikiliza.

Wapigieni nyote

Mbiu na sauti kuu.

Mungu katupa sote

Motto wa mbinguni,

/: kwa kutupenda sisi

Amekuja kwetu. :/

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu