86. Roho Yangu Tua Hapa



Roho yangu tua hapa

Mlimani pa Golgota,

Angalia tendo hili,

Afanyalo mfalme mkuu.

Amevutwa na upendo

Kuacha enzi yake.


Yesu alivyotupenda,

Twaona msalabani,

Maumivu hata manza

Ya makosa yampata.

Anakaa mahali petu,

Sikia ateswavyo!


Kufa kwako kunivute

Nife pamoja nawe

Mwili na mapenzi yangu

Yakazikwe nawe Bwana.

Niwe na kutengemana,

Mwenye pendo la kweli!

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu