7. Moyo Wangu Sikiliza
Moyo wangu sikiliza
Habari njema hii
Ya wokovu mkubwa.
Sikia kuimbwa kwao
Malaika na watu:
“yesu azaliwa.”
Mponya amekuja leo
Kutoka mbinguni,
Aokoe watu.
Mungu wetu ameshuka,
Akawa mwana mtu
Kwa ajili yetu.
Na sasa yumo zizini,
Aita: “njooni
Hima kwangu wote,
Nawaondolea ninyi
Uchungu wowote,
Muwe na furaha.”
Basi tumwendee hima
Wakumbwa wadogo,
Njooni wote sasa!
Awe mwanga wetu.
Wenyeshida na ukiwa njooni,
Awape neema yake Mungu,
Yeye ana mali nyingi,
Dhahabu na fedha
Za mioyo yenu.
Ninakaa ulimwenguni
Lakini napenda
Kuhamia kwako.
Mwisho niwe furahani
Pamoja na wewe
mwenye utukufu.
Comments
Post a Comment