48. Yesu Mponya tu Hapa



Yesu mponya tu hapa,

Moyo watulia,

Mawazo yetu yote

Uyavute kwako.

Mwanga wa neno lako,

Utuangaze wote,

Tuwe na mwangazo.


Kaa karibu na sisi,

Tunakutamani,

Mfunzi wetu ni wewe,

Sisi wanafunzi.

Nenolo lina nguvu,

Litatufanya wapya,

Laongoza vema.


Tuna furaha kubwa,

Tunakungojea.

Wewe u mwamba wetu

Tutegemeao.

Bwana tunakushika

Mpaka tunapofika

Uzimani kwako.

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu