117. Yesu Amefufuka (Haya Shangilia)
1. K: Yesu
W:Amefufuka, ametoka kaburini
K: Haya,
W: Shangilia,
K: Haya,
W: Shangilia, ametoka kaburini.
2. K: Shetani
W: AMeshindwa.
K: Shetani
W: Ameshindwa hana lake duniani
K: Haya,
W: shangilia,
K: Haya
W: Shangilia, ametoka kaburini.
3. K: Yesu
W: Kawatokea,
K: Yesu
W: Kawatokea wanafunzi wake wote
K: Haya,
W: Shangilia
K: Haya
W: Shangilia ametoka kaburini.
4. K: Amani
W: Iwe kwenu,
K: Amani
W: Iwe kwenu Mpokee Roho wangu.
K:Haya,
W: Shangilia,
K: Haya
W: Shangilia, ametoka kaburini.
5. K: Bwana
W: Yesu kapaa, sasa yu juu mbinguni
K: Haya,
W: Shangilia, sasa yu juu mbinguni.
6. K: Sasa
W: Kristo huketi,
K: Sasa
W: Kristo huketi kuumeni mwake Baba
K: Haya,
W: Shangilia,
K: Haya
W: Shangilia, sasa yu juu mbinguni.
7. K: Hivyo
W: Anatawala,
K: Hivyo
W: Anatawala pamoja na Baba yake,
K: Shangilia,
K: Haya
W: Shangilia, sasa yu juu mbinguni.
8. K: sisi
W: Tusiogope
K: sisi
W: Tusiogope, amemtuma roho wake,
K: Ili
W: tuwezeshwe,
K: Ili
W: Tuwezeshwe kuwa mashahidi wake.
9. K: Siku
W: Twaingojea
K: Siku
W: Twaingojea ya kurudi kwake Yesu.
K: Kweli
W: Tutaona,
K: Kweli
W: Tutaona, utukufu wake Bwana.
Comments
Post a Comment