56. Mmoja ni Mfalme
Mmoja ni mfalme shujaa,
Ni mshindaji!
Enyi adui, kimbieni tu!
Nawe Sayuni uone furaha
Ukapumzishe kabisa moyo:
Uzima, utengemano, furaha
Ndizo Mwokozi
Atakazokupa.
Twende kuonja maji ya uzima
Tunayopewa na Bwana Yesu,
Aliyesema
‘’Njooni kwangu wote,
Nitapumzisha mioyo yenu’’
Nyweni, wapenzi, katika
Kisima
Chenye wokovu wa wenye
Huzuni.
Mfalme wa mbigu
Ataka kuwapa
Kilemba kizuri cha urembo,
Awawekea viti vya milele,
Heshima hiyo ni ya kushinda.
Vumilieni tabu na shida:
Yesu mwenyewe ni tuzo la
Vita.
Nguvu, ujuzi, heshima
Na sifa
Ni zake Mungu na Mwamwa
Wake.
Name nataka kufika
Mbinguni!
Nifunguliwe mafungo yangu!
Mwenye upendo atanisikia.
Wenye uzima wanamsifu
Mungu.
Comments
Post a Comment