114. Amefufuka Katika Wafu



1. K: Amefufuka katika wafu, akiwa na utukufu. 

Kristo pekee, ndiye mwenye nguvu. 

W: Yeye limbuko la waliolala, 

tena ni mwisho wa nguvu ya mauti kwetu.


2. K: Hii ni habari iliyo kweli, iletayo udhahiri.

 Yapasa wote, tuache mashaka. 

W: Yesu pekee ndiwe ustahiliye kushika mamlaka yote.


3. K: Kristo u Bwana mwenye uweza. 

Shetani umemshinda, kazi yote umeimaliza. 

W: Uhimidiwe, ewe Bwana pekee, utupokee tunapokuja kwako, Bwana.


4. K: tuutangaze ushindi wake,

mataifa waje kwake, 

wafahamu utukufu wake. 

W: Asante, Bwana, kwa ushindi wako kwa watu wako. Shetani hana nguvu tena.


Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu