11. Natoka Leo Mbinguni



Natoka leo mbinguni

Naleta habari njema

Habari yenye furaha

Kwaninyi na watu wate.


“Amezaliwa kitoto

Na mwana mwali Maria,

Nimototo mzuri na mwema,

Awaletea furaha.”


Ni Yesu, mwana wa Mungu,

Mwokoxi wa ulimwengu

Atakae kuondoa

Makosa yote na shida


Awapa wote wokovu

Ulio wekwa naMungu

Make nanyi mbinguni

Pamoja nasi milele


Alama yenu iwe hii;

Zizini mototo wa maskini

Alie vikwa viguo,

Nae ni Bwana wa mbingu


Tumsifuni sisi sote,

Tuwafuate wachunga,

Tuyaone yale makuu,

Tulio pewa na Mungu.


Yesu unipendezae,

Ugeuze moyo wangu,

Uwe nyumba yako nzuri,

Nisikuwache daima.


Tumsifu bwana wa mbingu,

Alie mtoa mwanawe.

Tumimbie kwa furaha

Pamoja nao malaika.

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu