79. Nakusalimu Kichwa



Nakusalimu kichwa

Kilichojaa damu,

Kilichovikwa taji

La miiba mikubwa,

Kilichopata enzi

Kwa Mungu mbinguni,

Kitukanwacho sasa

Matusi makali.


Naona uso wako watemewa mate,

Watemewa mate,

Heshima yako yote

Imeondolewa.

Mwanga wa macho yako

Wazimika sasa.

Aliyekuharibu hivi,

Ndiye nani?


Mateso yako Bwana,

Yanipasa mimi.

Wewe waadhibishwa

Kwa ajili yangu.

Hukumu unapata iliyonipasa.

Bwananangu nakuomba,

Unihurumie!


Na mimi nasimama msalabani pako;

Niwe karibu kwako utoapo roho;

Ukiugua sana kwa teso la kufa,

Nitakushika Bwana

Kwa moyo wa pendo.


Bwana nayashukuru

Masumbuko yako,

Sababu ya kuteswa

Na kufa kuchungu.

Wewe umenishika,

Nami nakushika,

Mwisho nitakufia

Uliyenifia.


Moyo unaposhikwa

Na woga wa kufa,

Usiniache Bwana

Katika vita hii.

Siku ya kufa kwangu

Unisaidie,

Kufa kwako kuchungu

Kutaniokoa.


Niwie kama ngao

Nitakapo kufa,

Nione uso wako

Katika uchungu.

Ndipo nikutazame

Nikukumbatie!

Anaye kufa hivi

Afa kwa amani.

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu