92. Ukiwa na Vichache
N.K. 73,. H.C. 96 Mtunga sauti. S. Salvatori
Ukiwa na vichache umtolee Bwana,
kwani akiba yako ataiongeza.
Vipaji vyako haba yeye hakatai,
kidogo kwako wewe, kwake kitazidi!
Vile vile na moyo umtolee Bwana!
Ndivyo vipaji vyema vinavyompendeza.
Kwani sisi wenyewe alitukomboa,
akiuawa yeye kwa kuwambwa mtini.
Ukiwa na ubaya umwambie Bwana!
Ukishindana nao, atakutakasa.
Damu aliyotoa, ndiyo itoshayo,
kuosha wakosaji, hata wewe vivyo.
Vitu vya mali nyingi umtolee Bwana!
Alitoka mbinguni kusumbuka hapa.
Alikufa mwenyewe kwa ajili yako,
nawe hutoi chako kwa ajili yake?
Wakristo na tutoe shukrani kwa Mungu.
Hiyo ndiyo shukrani ya wokovu wetu.
Injili yake Kristo, ienee pote!
Kwa ushuhuda wetu watu waokoke.
Comments
Post a Comment