107. Kumekucha, ni Mzima
Kumekucha, ni mzima Yesu
aliyefufuka. Kaburi lake wazi,
kufa hakumshiki Yesu.
Sina woga na kifo, Yesu amefufuka.
Kumekucha, ni mzima Yesu aliyefufuka!
Tunaitwa nduguze, sababu anatupenda.
Tusiachane naye, yeye aliyeshinda.
Kumekucha, ni mzima Yesu aliyefufuka.
Kamba zitufungazo zimekwisha
funguliwa mwili wangu uoze,
sina woga na kufa!
Comments
Post a Comment