110. Haleluya, Haleluya



Haleluya, Haleluya,

sauti na mioyo juu,

tumwimbie Mungu nyimbo

tumsifu na furaha, aliyemwaga

damuye kwa ulimwengu wote,

mefufuka kifoni sas Yesu Mwokozi.


Minyororo yake kifo imekatika

pia, na katika wafu wote

yee mzaliwa wa kwanza Yesu

ameshinda sasa, nasi twashinda

naye. Ametupatia nasi

uzima wa milele.


Kristo afufuka kwanza nao

wengi baadaye. Atakapokuja tena,

watatokea naye, mavuno yatakuwako

mwisho wa ulimwengu,

watafika furahani wote watakatifu.


Mwokozi amefufuka, nasi tutafufuka,

tunyeshee kama mvua neema yako ee Bwana.

Tutafute yaliyo juu, siyo ya ulimwengu,

na uzima tutapewa naye Kristo kwa Mungu.


Tumsifu, tumsifu Mungu wetu, apaswa.

Tumsifuni na Mwokozi, aliyeshinda vita.

Tumsifu naye Roho, kisima cha mapenzi.

Tumsifu Mungu wetu, ni Utatu wa enzi.

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu