21. Watoto Njooni Bethlehemu
Watoto njooni,
Bethlehemu,
Njooni zizini kuona makuu
Mungu aliyotutendea leo,
Watoto waone furaha
Kubwa.
Twaona kitoto kizuri
Hapa, wazee wamtazama,
Wanafurahi?
Wachungaji wote
Wanangukia,
Malaika wa mbingu
Wanamwimbia.
Pigeni magoti na
Wachungaji!
Wakubwa, wadogo
Tumnyenyekee!
Sasa popote patengenezwe,
Na watu wote watapendezwa.
Furahini!
Tuimbe na sisi kwa
Furaha kuu
Nyimbo za kumsifu
Mwokozi Yesu!
Watoka mbinguni
Utuokoe,
Waona uchungu sababu
Yetu,
Leo wazaliwa na mwana
Kikiwa.
Halafu wateswa, unatufia.
Twapenda kukupa mioyo
Yetu,
Twataka kukutumikia vema.
Takasa mioyo ikupendeze,
Tupate kufika kwako
Mbinguni.
Comments
Post a Comment