6. Wakristo, Iwekeni


Wakristo, iwekeni

Mioyo tayari.

Yesu awaingie,

Ni Mwokozi wenu.

Mungu amemtuma

Kwa neema na rehema

Atuletee sisi

Uzima na nuru.


Mwokozi ana kuja,

Mlimieni njia!

Mioyo iwe safi

Acheni matendo

Yanayomchukiza.

Lijazwe kila bonde,

Milia ipunguzwe

Mioyoni mwenu.


Ukiwa mnyenyekevu,

Wapendwa na Mungu.

Ukiwa na kiburi,

Utaangamizwa.

Ukimtumikia,

Mungu kwa mwendo mwema

Umpendezao yeye,

Yesu akupenda.


Uniweke tayari

Niliye maskini,

Ee Yesu siku hizi

Kwa rehema yako

Ingia moyoni,

Ukinijia sasa.

Nami nitakusifu

Kwa kinywa na moyo.

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu